• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKUU WA WILAYA AMPONGEZA MTENDAJI KIHAGARA

Posted on: February 26th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, amempongeza Afisa Mtendaji wa kata ya Kihagara Eva maendaenda,  kwa kuwarudisha  shuleni watoto wawili waliokuwa wakitumikishwa kufanya kazi za ndani Mkoani Dodoma, na kuhakikisha wanaendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Mango.

Pongezi hizi amezitoa hivi karibuni wakati akitoa salamu za Serikali, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa lilichofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba, mjini  Mbamba-bay Wilayani hapa.

Bi Chilumba alimpongeza Mtendaji huyo kwa kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wameripoti Shuleni kwa asilimia mia moja, na kuanza masomo, licha ya watoto wengine wawili, wakishirikiana na wazazi wao, ambao walipelekwa Dodoma kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, lakini Mtendaji alihakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria wazazi/walezi ambao watoto wao walikuwa wakitumikishwa kwa kazi za ndani, Hivyo    wanafunzi hao wamerudishwa, wako shuleni na wanaendelea na masomo.

“Nichukue Fursa hii kumpongeza sana Afisa Mtendaji Kata ya Kihagara na Kamati nzima  ya Maendeleo ya Kata ya Kihagara, kwa kuwarudisha wanafunzi wawili waliokuwa wakitumikishwa kazi za ndani Mkoani Dodoma, kwa kuwarudisha na kwa sasa wanaendelea na masomo, katika shule ya Sekondari ya Mango Wilayani hapa. Nahitaji Watendaji wote muige  Mfano wa Mtendaji wa Kihagara. Kama ameweza kuwatoa watoto Dodoma na kuwarudisha shule wewe, wanafunzi unao katika eneo lako la utawala kwa nini Wasiende shule? Nahitaji wanafunzi wote waripoti kwa asilimia mia moja ifikapo Februari 29 mwaka huu. Alisema Chilumba.

Aidha aliwaagiza madiwani na Watendaji  wa Kata kuhakikisha wanasaidiana na wakuu wa shule, kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika shule hizo kwa kuwa mwaka huu ,kuna changamoto chanya ya kupokea wanafunzi wengi zaidi kuliko miaka iliyopita.Hivyo changamoto ya Madarasa na meza zitatuliwe   mapema kama walivyoanza kutatua changamoto hizo.

Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Kihagara alitaja mbinu alizotumia ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti ni, kutoa Elimu kwa wazazi/ walezi na watoto, tangu wanapomaliza elimu ya Msingi kwa kuwaambia kuwa bado ni wanafunzi na hawaruhusiwi kufanya chochote isipokuwa ni kujiandaa na kuendelea na masomo ya Sekondari, hali inayowafanya wahitimu hao kusubiri kwenda shule. Njia nyingine ni kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wasiowapeleka shule watoto wao.

Aliongeza kuwa Ushirikiano anaopata kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Kihagara, Mh George Ndimbo na wajumbe wake na Viongozi wa Vijiji ndio unaompelekea kufanikisha Malengo yake aliyojiwekea.

Mh.Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akitoa  hali ya Uripoti wa wanafunzi wa Sekondari alisema mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 2813 ambao ni sawa na asilimia tisini (90%) wameanza masomo katika shule zote za Serikali na akawaagiza Maafisa watendaji kata wote kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu 2020 wanaripoti kwa asilimia (100%).

Imeandaliwa na Netho C.Sichali

Kaimu Afisa habari (W) Nyasa 0767417597

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • Tangazo la Mikopo October 09, 2025
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Maonesho ya Nane Nane Kanda za Nyanda za juu kusini , Mguu sawa Kuanza leo

    August 01, 2025
  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.