• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKUU WA WILAYA AHAMASISHA UJENZI WA KITUO CHA POLISI CHA TARAFA YA MPEPO

Posted on: July 17th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, hivi karibuni amefungua rasmi  Ujenzi wa Kituo cha Polisi  cha Tarafa ya Mpepo kinachojengwa katika Kata ya Tingi Wilayani Nyasa.

Akifungua Ujenzi huo  katika eneo la ujenzi, aliwahamasisha wananchi waweze kuchangia Ujenzi huo, na  kufanya harambee ya kukusanya michango, ili kuhakikisha ujenzi unaanza kwa haraka na kukamilika ndani ya mwaka huu 2020.

Chilumba alifafanua kuwa lengo la kuhamasisha ujenzi wa kituo cha polisi katika Tarafa ya Mpepo,  ni kuimarisha Ulinzi katika maeneo ya Mpakani kwa kuwa Tarafa hiyo inapakana na Nchi Jirani ya Msumbiji, hivyo waarifu wengi wanaweza kuingia au kutoka katika Tarafa  ya Mpepo.

Aliongeza kuwa Wananchi wanatakiwa kuhamasika, kuchangia mradi  wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Katika Tarafa ya Mpepo, ili Raia wa Tarafa hiyo na mali zao ziwe salama wakati wote ili kuleta maendeleo, katika ngazi ya kaya, na Tarafa kwa ujumla kwa kuwa Polisi watafanya kazi na watatoa Huduma kwa masaa 24 tofauti na ilivyokuwa sasa, Kituo kinachotoa Huduma ni kidogo na Polisi ni  wachache wanaofanyakazi katika Kituo Cha Polisi.

“Ndugu wananchi wa Tarafa ya Mpepo leo nimefika hapa kufungua na kuhamasisha, ujenzi huu wa kituo cha Polisi cha Tarafa hii Utaona leo Serikali ya Wilaya iko Mahali hapa, ,Mimi Mkuu wenu wa Wilaya niko Hapa na Wakuu wa Idara na Vitengo wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wote wako hapa kwa lengo la kuhamasisha na kuchangia ujenzi wa Kituo hiki. Lakini leo lazima tuanze rasmi ujenzi wa kituo hiki, tutakwaa na kuseti msingi na tutaanza kuchimba Msingi.Lengo la kujenga Kituo hiki ni kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Tarafa hii kwa kuwa inapakana na Nchi jirani ya Msumbiji”. Alisema Chilumba

Wananchi wa Tarafa ya Mpepo walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba kwa kuhamasisha  ujenzi huo  na kumuahidi kuwa watajitoa kwa moyo na kweli wana uhitaji wa kituo hicho hivyo wameona nia ya Serikali Wilayani Nyasa ni kuona Raia wake wanaishi kwa amani hivyo watahamasisha ujenzi huo.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.