• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKUU WA MKOA AIPONGEZA NYASA

Posted on: June 12th, 2019


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

Alizitoa Pongezi hizo wakati akihutubia baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa lililofanyika jana katika Ukumbi wa Kepten John Komba uliopo katika Mji wa Mbamba-Bay Wilayani Nyasa akiwa katika Ziara ya kikazi ya Siku moja ambayo alihudhuria kikao cha Baraza la Madiwani na kukagua Miradi ya maendeleo.

Mndeme alifafanua kuwa Ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali ni matakwa ya Kikatiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya mwaka 1977 na kufanyiwa marekebisho ya mwaka 2005 kanuni namba 10 ya sheria ya ukaguzi namba 11 ya mwaka 2008.

Aliongeza kuwa Ukaguzi huu upo kisheria ni haki yetu kukaguliwa na Msipokaguliwa mna haki ya kuhoji kwa nini hamjakaguliwa, kwani hoja zinawahusu wote yaani Madiwani na wa tendaji kwa vile Halmashauri ina undwa na pande zote mbili.

Aidha alimpongeza Mhe. Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Martin Manyanya, Madiwani na Wataalam wote wa Wilaya ya Nyasa kwa kusimamia vema matumizi ya fedha za miradi na kupata Hati safi kwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2017/2018, na kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2017/2018.

“Halmashauri hii imeshakaguliwa na CAG kwa miaka mitano kuanzia mwaka wa Fedha 2013/2014-2017/2018 katika kipindi hiki chote Halmashauri imepata Hati safi mara nne (4)na kupata hati yenye mashaka mara moja Hongereni sana kwa hati mnazoendelea kupata.hii ni matokeo ya utendaji kazi mzuri wenye mshikamano na ushirikiano.Inapotokea mmefanya vizuri hata sisi viongozi katika ngazi ya Mkoa tunafarijika sana kuona Halmashauri zetu zinafanya vizuri. Pia niwakumbushe pia msibweteke na kuona mmefika mwisho bali kwa mwaka unaofuata mzuie hoja sio kuzalisha hoja”.alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika Hatua nyingine Alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Jimson Mhagama kwa kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa na kumtaka ashirikiane na Madiwani, Wataalumu na Wananchi ili Wilaya iweze kuwa na Maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mh. Alto Komba alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kwa kufanya ziara ya siku moja Wilayani Nyasa na kuhudhuria Baraza la Madiwani na kusema kuwa wananyasa wamefarijika sana kwa ujio wake na wanamkaribisha siku nyingine akipata nafasi.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme alifanya ziara ya siku moja wilayani hapa na kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa na kukagua Miradi Mitatu ya Maendeleo .Miradi hiyo ni Jengo Ofisi na nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Jengo la Hosteri ya wasichana Limbo sekondari,na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

IMEANDALIWA NA

KITENGO CHA TEKNOLOJIA YA

HABARI NA MAWASILIANO

WILAYA YA NYASA.

0759745514

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.