• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKUU WA MKOA AHAMASISHA JAMII KUACHA UKATILI WA KIJINSIA

Posted on: March 9th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme, ameitaka jamii kuacha ukatili wa kijinsia, na wahamasike  kuongeza fursa za Kiuchumi kwa Wanawake kwa kuwajengea  uwezo wa kitaalam, kibiashara, na mbinu za kupata mtaji na masoko.

Aliyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wanawake, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kimkoa yaliyofanyika katika Viwanja vya Polisi ,Mjini Mbamba-bay Wilayani hapa.

Mndeme aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, alifafanua kuwa, jamii inatakiwa kuacha mara moja Ukatili wa kijinsia, na badala yake wahamasike kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake,kwa kuwajengea uwezo wa kitaalam, kibiashara, na mbinu za kupata mtaji wa masoko ili waondokane na utegemezi.

Aliongeza kuwa,  Serikali na wadau kwa ngazi zote, haina budi kuendelea kuweka vipaumbele vya kuwainua Wanawake  Vijijini, ili waweze kuwa Wajasiliamali wenye bidhaa bora na kuwatafutia masoko ya Kimataifa kwa lengo la kuitangaza nchi yetu, na kuinua uchumi wa Taifa letu.

“jamii haina budi kuongeza fursa za Kiuchumi kwa Wanawake ili kuwajengea uwezo wa kitaalam, kibiashara, mbinu za kupata mtaji na masoko. Serikali na wadau na ngazi zote kuendendelea kuweka vipaumbele vya kuwainua Wanawake  Vijijini waweze kuwa Wajasiliamali wenye bidhaa bora na kuwatafutia masoko ya Kimataifa kwa lengo la kuitangaza nchi yetu lakini vilevile kuinua uchumi wa Taifa letu.

 

Naye mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Bi Zawadi Nyoni , akitoa maelezo ya idara yake alisema , amewahamasisha wanawake wengi kujiunga na kuanzisha vikundi vya wanawake ili kuvipatia mikopo mbalimbali, na hadi Desemba 2019 jumla ya vikundi vya wanawake 389 vimeundwa na kukopeshwa tsh 509,174,487.00 ikiwa ni fedha za asilimia kumi za mapato ya ndani za Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma.

Bi Nyoni aliongeza kuwa idara yake inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii, uhaba wa vitendea kazi ikiwemo usafiri, kutopewa fedha za asilimia kumi kwa wakati na hata zikipatikana hazikidhi mahitaji ya waombaji wa mikopo.

Maadhimisho hayo yameambatana na shughuli mbalimbali zilizofanyika Wilayani hapa, ikiwa ni pamoja na Kongamano la Wanawake wajasiliamali ambapo walipewa elimu ya ujasiliamali na elimu ya kuzifahamu haki na Sheria za ndoa na Mirathi, pamoja na kutembelea na kutoa misaada mbalimbali katika wodi ya wazazi (Maternity) katika kituo cha afya cha Mbamba-bay Wilayani Nyasa.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni sabuni ya unga mifuko mitatu,buti pea tisa, sabuni za mche katoni tatu, mpira ya kutandika kitandani meta nane, brash za kufanyia usafi 6, Ndoo za taka 06, ndoo za kudekia 04.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.