• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKURUGENZI UCHAGUZI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WASIMAMIZI NGAZI YA JIMBO MKOANI RUVUMA

Posted on: October 19th, 2020



Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Charles amewaagiza wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Dkt.Charles ametoa agizo hilo wakati anafungua mafunzo ya uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo Kanda ya Ruvuma yenye mikoa ya Njombe, Ruvuma,Mtwara,Lindi,Iringa na Mbeya.Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

“Kama unavyoona Taifa letu sasa hivi kuna baadhi watu  wanachokochoko sana,kwa hiyo mjitahidi kufanya kazi kwa kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka shari ya watu hao’’,alisisitiza Dkt.Charles.

Amesema hadi sasa NEC imeshatuma sehemu kubwa ya vifaa vya kufanikisha uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu na kwamba vifaa hivyo vimekwishaanza kusambazwa na inatarajiwa hadi kufikia Oktoba 24 kila Halmashauri nchini itakuwa imepokea vifaa vyote vya uchaguzi.

Amewashauri wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo kuanza kuvipakua vifaa hivyo na kuvisambaza katika maeneo yote na kwamba wasisubiri hadi Oktoba 27.

“NEC katika uchaguzi wa mwaka huu tunataka kuwa tofauti ukilinganisha na mwaka 2015,kwanza serikali imetuletea fedha zilizotokana na kodi za walipa kodi  kwa wakati,hivi tunavyoongea zaidi ya shilingi bilioni 120 nimezishusha ngazi ya Halmashauri’’,alisisitiza Dkt.Charles.

Amewataka wasimamizi hao kufikisha vifaa vya uchaguzi ngazi ya Kata kwa wakati ili wale ambao wamezoea kulalamika kuwa NEC imechelewa kufungua vituo na kuchelewesha vifaa katika uchaguzi wa mwaka huu wakose cha kusema.

Kwa mujibu wa Dkt. Charles,kuanzia Oktoba 24 hadi 26 NEC itaanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo,wasimamizi Wasaidizi wa vituo na makarani waongozaji.

“Wasimamizi wa majimbo,mnatakiwa kuyapa umuhimu mkubwa na wa kipekee mafunzo haya hasa kwa kuzingatia kuwa watendaji mtakaowafundisha ndiyo watakaosimamia zoezi la upigaji kura na kuhesabu kura vituoni’’,alisema Mkurugenzi wa NEC.

Dkt.Charles pia amewaagiza wasimamizi wa majimbo kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa ifikapo Oktoba 21 mwaka huu na kusisitiza kuwa  vyama vya siasa ambavyo vitaleta mawakala muda ukiwa umekwisha, mawakala wake hawataapishwa na hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura.

Mkurugenzi huyo wa NEC amesema daftari la kudumu la wapigakura  lina jumla ya wapigakura milioni 29,188,347 na kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutakuwa na vituo 81,567 vya kupigia kura kwa nchi nzima.

Amesisitiza kuwa baada ya wapigakura, kupiga kura zao sheria inawataka  kuondoka vituoni na kurudi nyumbani kusubiri matokeo. na kwamba hakuna sheria inayosema wabaki vituoni.

Gaspar Balyomi ni Msimamizi wa Uchaguzi  Jimbo la Tunduru,akizungumza baada ya kupata mafunzo hayo ameahidi kusimamia maelekezo yote ya NEC ili kuhakikisha wananchi wanapiga kura katika vituo husika kwa uhuru na kurudi nyumbani kusubiri matokeo.

Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbinga Mji Grace Quintine amesema mafunzo hayo yamewakumbusha kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi tangu kuanza kwa mchakato wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 19,2020


Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.