• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MITI YA MITIKI ITAKAVYOTENGENEZA MAMILIONEA WILAYA YA NYASA

Posted on: December 9th, 2020


Miti ya mitiki itakavyotengeneza mamilionea wilaya ya Nyasa

Programu ya kuendeleza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (FORVAC) imetoa ruzuku ya miche ya mitiki zaidi ya 81,000 iliyopandwa katika hekta 72.1 kwa wakulima 80  mwambao mwa Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma msimu wa mwaka 2019/2020.

Mwenyekiti wa Muungano wa Chama  cha Wazalishaji wa miti ya misaji (mitiki) kijiji cha Liuli wilaya ya Nyasa Samwel Mawanja amesema  FORVAC wanaendelea kufadhili mradi wa miti ya mitiki ambayo inatekelezwa katika vijiji sita mwambao mwa ziwa Nyasa.

“Katika msimu wa mwaka 2020/2021 tumeomba tena FORVAC ruzuku ya miche ya mitiki 300,000 kupitia vijiji sita vinavyozalisha mitiki ambavyo ni Liuli,Nkalachi,Nkali A,Nkali B na Lipingu na Hongi’’,alisema Mawanja.

Amesema mradi wa mitiki ni mradi pekee ambao haujawahi kutekelezwa tangu uhuru mwambao mwa ziwa Nyasa ambao unatarajia kuleta tija kubwa kiuchumi kwa wananchi hivyo kuleta mapinduzi makubwa kiuchumi baada ya miti hiyo kuanza kuuzwa.

Ameyataja matarajio ya wananchi hao ambao pia ni wavuvi katika ziwa Nyasa kuwa ni kutengeneza boti za kisasa kwa kutumia miti ya mitiki zitakazowawezesha kwenda kuvua mbali badala ya kuendelea kuharibu misitu ya asili kwa kukata miti ya kutengenezea mitumbwi.

Kwa upande wake Mratibu wa  FORVAC Taifa Emanuel Msoffe akizungumza baada ya kukutana na kikundi hicho cha wazalishaji mitiki,ametoa rai kwa wananchi mwambao mwa ziwa Nyasa kulinda na kuhifadhi misitu iliyopo kwenye milima ya Livingstone kwa kuacha kulima na kukata miti hovyo.

Amesisitiza kuwa eneo la Mwambao mwa ziwa Nyasa linafaa sana kwa uzalishaji wa mitiki kwa sababu ni eneo ambalo lipo chini ya milima ya livingstone hivyo lina  rutuba nyingi.

“Natoa rai kwa wananchi mwambao mwa ziwa Nyasa kuendelea kupata miti ya mitiki kwa sababu kati ya miaka 15 hadi 20 mtavuna na kupata fedha nyingi zitakazobadilisha kabisa maisha yenu’’,alisisitiza Msoffe.

Ofisa Maliasili wa Halmashauri ya Nyasa Bugingo Bugingo amesema utafiti umebaini kuwa hekari moja ya mitiki inaweza kumuingizia mkulima zaidi ya milioni 400 hivyo ni muhimu wananchi kupanda miti hiyo ili kukuza uchumi wao.

Bugingo anayataja miongoni mwa matumizi ya zao la mitiki  ni kutengenezea vitako vya silaha aina ya bunduki,vyombo vya majini kama vile meli na boti na kutengeneza samani mbalimbali zenye gharama kubwa.

Utafiti umebaini kuwa Mahitaji ya mtiki katika soko la duniani ni makubwa ,ndiyo maana nchi za Ulaya na nchi za Asia zikiongozwa na China na India wananunua miti aina ya mitiki kwa wingi kutoka Tanzania,na hata hatujaweza kufikisha hata robo ya mahitaji yao.

Nchi  ya Malyasia kwa mwaka hupata mapato ya Dola  za Marekani zaidi ya bilioni 13 kutokana na kilimo cha mitiki.Mahitaji ya soko la mitiki ni makubwa hivyo wakulima wapya wa mitiki katika wilaya ya Nyasa na maeneo mengine nchini waongeze uzalishaji wa zao hili,  mahitaji yake yanaendelea kuongezeka



Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.