• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

Posted on: June 19th, 2025

Na Byarugaba Innocent, Nyasa DC

Ikiwa imesalia siku moja, kabla ya kuvunjika kikanuni kwa mabaraza ya Wahe. Madiwani nchini kama ilivyotangazwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Mohamed Mchengerwa Juni 20, 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imefanya tafrija ya kuwapongeza madiwani wake kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuisimamia Halmashauri ndani ya Miaka Mitano.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Khalid Khalif amewashukuru Wahe. Madiwani kwa uongozi wao shirikishi wa kuisimamia Halmashauri na kuiwezesha kupata mafanikio makubwa ndani ya miaka mitano ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa makusanyo ya Halmashauri kutoka wastani wa bilioni 1.4 mpaka kufikia wastani wa bilioni tatu kwa mwaka huku miaka yote Halmashauri ikijinyakulia hati safi.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Walarick Kilasi amesema kufanyika kwa hafla hiyo ni matokeo ya mafanikio yaliyofikiwa katika halmashauri ya Nyasa yanayotokana na kufanyakazi kwa kuheshimiana, kushikamana na ushirikiano baina ya Chama cha Mapinduzi, Wahe. Madiwani na Wataalam kwani mara zote wameendelea kuongea lugha moja wanapokuwa kwenye agenda za mapato na matumizi hata leo tunafanya tafrija hii yak upongezana tukiwa tunaongea lugha moja ya mapato na maendeleo kwa wananchi wetu wa Nyasa

Salum Ismail, Katibu tawala wilaya ya Nyasa aliyekuwa mgeni rasmi katika tafrija hiyo amewapongeza Wahe. Madiwani kwa kuisimamia vema halmashauri  na kuweza kufikia kiwango kizuri cha mapato yaliyowezesha kutoa huduma stahiki kwa wananchi na kwamba mafanikio yanayoonekana leo ndani ya Nyasa yanatokana na mchango mkubwa uliotokana na wahe. Madiwani hasa katika kusimamia na kuminya mianya ya upotevu wa mapato kwenye vyanzo vyake.

Aidha, Ismail amewataka wahe. Madiwani kuingia kwenye kinyang’anyiro tena wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuinyanyua Halmashauri yao kimapato, Kujenga miundombinu ya afya, elimu, maji, Barabara na kuiwezesha Halmashauri kutoa asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyowezesha vikundi vya akina mama, Vijana na wenye ulemevu kujiajiri na kuboresha maisha yao kuanzia ngazi ya kaya.

Aidha, Ismail ametoa rai kwa Wahe. Madiwani kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali wakati wote kwani Mkuu wa Wilaya ataendelea kuwatumia kama Madiwani Wastaafu kama nyenzo ya utatuzi wa kero kwenye Kata na kwamba heshima na michango yao bado inahitajika.

Waheshimiwa Madiwani na wataalam wamekula na kunywa katika tafrija hiyo na kucheza muziki pamoja kama ishara ya kutakiana maisha mema baada ya baraza kuvunjika rasmi kikanuni hapo Juni 20,2025

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.