• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Mikoa ya Ruvuma, Njombe, Rukwa na Songwe kuanza uboreshaji wa Daftari la wapiga kura tarehe 12-18 January 2025

Posted on: December 31st, 2024

Mikoa ya Ruvuma, Njombe, Songwe na Rukwa kuboresha daftari la wapiga kura Januari, 2025.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe, Songwe na Rukwa ambapo zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 12 hadi 18 Januari, 2025.

Hayo yameanishwa kwenye hotuba ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jacobs Mwambegele iliyosomwa kwa niaba yake kwenye mikutano  ya Tume na  wadau wa uchaguzi iliyofanyika leo tarehe 31 Desemba, 2024 kwenye  mikoa ya Ruvuma, Njombe, Songwe na Rukwa.

Mhe. Mwambegele ambaye aliwakilishwa na wakurugenzi mbalimbali wa Tume kwenye mikutano hiyo,  amesema mikoa hiyo itafanya uboreshaji kwenye mzunguko wa tisa na kwamba tayari Tume imekamilisha uboreshaji kwenye mikoa 19 ambayo ilijumuisha mizunguko nane kati ya mizunguko 13 ambayo imepangwa kukabilisha zoezi hilo nchini.

“Leo tupo hapa Songwe na wenzetu wapo kwenye mikoa ya Njombe, Rukwa na Ruvuma ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huu wa Songwe, Njombe, Rukwa na mkoani Ruvuma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Mbinga Mji, Wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea, zoezi litakalofanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 12 Januari, 2025 na kukamilika tarehe 18 Januari, 2025 na ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Ameitaja mikoa ambayo tayari imekamisha zoezi hilo kuwa ni Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma na Singida.

“Mikoa mingine ni mikoa ya Zanzibar ambayo ni Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha na Kilimanjaro. Kwa sasa mikoa miwili ya Mbeya na Iringa inatarajia kukamilisha zoezi hilo tarehe 02 Januari, 2025,” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Mada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani iliyowasilishwa kwa niaba yake kwenye mikutano hiyo imeanisha kwamba kwenye mikoa hiyo jumla ya wapiga kura wapya 475,743 wanatarajiwa kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Mada hiyo imeanisha kuwa uboreshaji wa Daftari utakapokamilika, mikoa hiyo inatarajiwa kuwa na  jumla ya wapiga kura  3,091,485 ikilinganishwa na idadi ya wapiga kura 2,615,742 waliokuwemo kwenye Daftari mwaka 2020.

“Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha,” imesema sehemu ya mada hiyo.

Mada hiyo imeanishwa kuwa kutakuwa na vituo 3,785 ikiwa ni ongezeko la vituo 233 kutoka vituo 3,552 vilivyokuwepo mwaka 2020.

Mwisho.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • Wilaya ya Nyasa yaadhimisha miaka 61 ya Muungano kwa Kufanya Usafi

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.