• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MIAKA 3 YA RAIS SAMIA WANANCHI NYASA WAMPONGEZA KWA UJENZI WA BANDARI

Posted on: March 20th, 2024

WANANCHI wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 12.2 kwa ajili ya ujenzi wa bandari mpya ya Ndumbi ziwa Nyasa.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza mjini Mbambabay amesema ujenzi wa bandari hiyo umekamilika kwa asilimia 100 na kwamba serikali pia imetenga shilingi bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya kisasa ya Mbambabay wilayani Nyasa.

“Kwa namna ya pekee tunamshukuru Jemedari wetu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mabilioni ya fedha kutekeleza miradi mikubwa ya bandari katika wilaya ya Nyasa’’,alisisitiza.

Manyanya amesema  serikali inaendelea kuifungua wilaya ya Nyasa katika sekta ya usafiri na usafirishaji hivyo kutoa fursa kwa wawekezaji kufika kuwekeza katika wilaya hiyo yenye fursa nyingi za kiuchumi na uwekezaji,

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Nyasa Manga Gassaya  akizungumzia utekelezaji wa ujenzi wa bandari ya Ndumbi,ameitaja miundombinu iliyojengwa katika bandari ya Ndumbi kuwa ni ujenzi wa Gati lenye urefu wa mita 160 kwenda ziwani na sehemu ya kupokea lango la meli yenye urefu wa mita 40.

Miundombinu mingine iliyojengwa katika bandari ya Ndumbi ameitaja kuwa ni ghala la kuhifadhia mizigo lenye mita za ukubwa 1,020,eneo la sakafu ngumu kwa ajili ya kuhifadhia mizigo isiyoathiriwa na mvua lenye mita za ukubwa 9030 na jengo la kupumzikia abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 70,000 kwa mwaka.

Gassaya amesema bandari ya Ndumbi baada ya kukamilika Desemba 2022 imeongeza uwezo wa kuhudumia shehena kwa bandari za ziwa Nyasa  kwa mwaka kutoka tani 76,000 hadi kufikia tani 110,000.

 Amesema bandari hiyo pia imeongeza uwezo wa kuhudumia abiria kutoka abiria 56,000 kwa mwaka hadi kufikia abiria 126,000.

Meneja huyo wa bandari za ziwa Nyasa amesema  serikali pia imeanza kutekeleza ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Mbambabay lengo likiwa ni kuimarisha ushoroba wa maendeleo ya Mtwara ambayo ni njia fupi na rahisi kuhudumia mizigo ya Malawi kutokea bandari ya Mtwara.

“Serikali ya Awamu ya Sita imetenga shilingi bilioni 70  kuanza kutekeleza mradi huo ambao unatarajia kukamilika ndani ya miezi 24,ujenzi wa bandari ya Mbambabay ukikamilika utaongeza uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo katika bandari  kutoka tani 110,000 hadi kufikia tani 550,000 kwa mwaka’’,alisema.

Hata hivyo amesema baada ya ujenzi wa bandari mpya ya Mbambabay kukamilika,makao makuu ya bandari za ziwa Nyasa yatahamia Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kutoka bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Amesema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika bandari za ziwa Nyasa,katika kipindi cha miezi  sita ya mwaka 2023/2024 bandari zimehudumia jumla ya abiria 7,358 na mizigo tani 1,828.6.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inasimamia bandari 15 katika ziwa Nyasa  zilizopo katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya na Njombe.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.