• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MGONJWA WA CORONA RUVUMA AMEBAKIA MMOJA, ANAENDELEA VIZURI

Posted on: May 19th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema hadi kufikia Mei 18,2020 Mkoa wa Ruvuma umebakiwa na mgonjwa mmoja wa corona  ambaye anaendelea vizuri.

Mndeme  ametoa taarifa hiyo wakati anazindua mpango wa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na ugonjwa homa kali ya mapafu katika Mkoa wa Ruvuma ulioandaliwa  na Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania(RED CROSS).

Amesema hali ya kupungua kwa wagonjwa wa corona katika Mkoa wa Ruvuma inaendelea vizuri ambapo katika vituo nane vilivyotengwa kwa ajili ya kuwalaza wagonjwa wa corona,amebakia mgonjwa mmoja tu ambaye ataruhusiwa baada ya muda mfupi kwa sababu anaendelea vizuri.

“Mgonjwa huyu mmoja anaendelea vizuri kwa taarifa nilizopata leo asubuhi,tayari ameanza kufanya mazoezi mwenyewe bila kupewa msaada na daktari,hizi ni juhudi zinazoendelea kufanywa na Mkoa ili kumuunga mkono Rais wetu katika vita ya corona’’,alisisitiza.

Ametoa rai kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania,wanapokwenda kutoa elimu ya umma dhidi ya corona kuhakikisha kuwa ,wananchi wanapata elimu itakayowaondoa hofu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi namna ugonjwa unavyoambukizwa na njia sahihi za kujikinga.

 Amesema Mkoa wa Ruvuma una jukumu la  kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita hii ya kupambana na Corona  kwa sababu amekuwa mstari wa mbele  kuhimiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga huku wakiendelea  kuchapa kazi .

Ameahidi kutoa ushirikiano na kwa RED CROSS  katika kuelimisha wananchi mkoani Ruvuma ambapo amewaagiza wakurugenzi katika Halmashauri zote kuhakikisha wananchi katika kata zote wanafikiwa na elimu hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania  Mkoa wa Ruvuma  Judith Kapinga amesema mradi huo ni kwa ajili ya kuelimisha jamii kujikinga na homa kali ya mapafu ya corona ambayo imekuwa inasumbua Dunia nzima.

 “Kazi yetu kubwa katika mradi huu ni kuelimisha jamii kuhusu corona,tumeteuliwa na Wizara ya Afya kwa sababu tuna watalaam wa kujitolea katika nchi nzima’’,alisisitiza.

Amesema katika Mkoa wa Ruvuma program hiyo itagusa kata zote 173 zilizopo katika Mkoa wa mzima wa Ruvuma na watafanya mafunzo kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambapo katika kila Halmashauri yatatolewa mafunzo kwa watu wa kujitolea 12 ambao watahusika na zoezi zima la uelimishaji.

Hata hivyo amesema uelimishaji huo utafanyika kwa mtindo wa kubandika  mabango,kugawa vipeperushi vilivyotolewa na Wizara ya Afya na kutumia vipaza sauti ambavyo vitakuwa na ujumbe maalum wa kukabiliana na virusi vya corona.

Amesema vipaza sauti hivyo vyenye uwezo wa kusikika meta 500 vitatumika kuelimisha katika maeneo yenye watu wengi ikiwemo stendi za mabasi,minada,kwenye vituo vya afya  na maeneo mengine yenye watu wengi,lengo likiwa ni kuhakikisha   elimu sahihi ya kukabilina na corona inawafikia wananchi wengi katika maeneo yote.

Hata hivyo amesema Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mkoani Ruvuma kimejipanga kuendelea na mafunzo hayo hata kama ugonjwa wa corona utatoweka nchini kwa sababu vifaa vya kutolea elimu vitaendelea kubaki katika maeneo husika na watalaam wataendelea kuwepo.

Naye Rais wa Chama Cha Msalaba Mwekundu  Tanzania David Kihenzile  ameutaja msingi wa kuanzisha chama hicho kuwa ni kusaidiana na serikali katika kutoa huduma za kibinadamu nyakati za vita ikiwemo njaa,ukame na magonjwa ya milipuko kama ilivyo sasa kwa mlipuko wa corona.

 Katika uzinduzi huo Chama hicho kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi  ya Corona ambavyo ni  vitakasa mikono,sabuni ya kunawia mikono na machine tatu za kunawia mikono.

Ugonjwa wa homa kali ya mapafu upo duniani kote ,unahitajika mkakati wa pamoja kwa ajili ya kukabiliana ikiwemo utoaji wa elimu sahihi kwa umma namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Mei 18,2020

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.