• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MARUFUKU KUTUMIKISHA WATOTO

Posted on: June 18th, 2019


 

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi Isabela Chilumba, amewataka wazazi na walezi kuacha kuwatumikisha watoto katika ajira mbalimbali na badala yake wawahimize kusoma kwa bidii ili kufikia malengo ya Serikali ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari.

Aliyasema hayo jana wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Nyasa katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kiwilaya yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Lundo, iliyopo katika Kijiji cha Lundo, Kata ya Lipingo, wilayani Nyasa.

Bi Chilumba alifafanua kuwa, maadhimisho ya Mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutambua haki za watoto, ikiwa ni pamoja na kuwatunza kuwalinda na kuwapa huduma zao zinazotakiwa katika jamii. Ikiwa watoto wanabaguliwa na hawapewi haki zao kama jamii, tunatakiwa kutoa taarifa katika ngazi mbalimbali za Uongozi ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Serikali za Mitaa, ili hatua zichukuliwe kwa wahusika wanao wanyanyapaa watoto.

Aliongeza kuwa, ili watoto tuweze kuwasaidia zaidi tunatakiwa kuwahimiza kupata elimu ya Msingi na Sekondari ambayo hutolewa bure na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kama wananchi tunatakiwa kumpongeza Rais wetu, Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha anatoa elimu bure na ili kumuunga mkono tunatakiwa kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule, waende shule na kuwalea watoto hao waweze kuwa na maisha bora, kwa kuwa Elimu itamsaidia kupambana na mazingira yake yanayo mkabili.

“Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mh. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha watoto wote wanapata elimu Bure, hivyo kama wazazi tunatakiwa kuhakikisha watoto wote walio na umri wa kwenda shule wanakwenda shule na kama kuna mzazi ambaye anawapeleka watoto wake katika ajira achukuliwe hatua mara moja. Huo ni moja ya unyanyasaji katika jamiii ambao hautakiwi na sio kusubiri tuu viongozi wafanye kazi hizo bali kila mwananchi anawajibu wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya unyanyasaji, ukatili, wanaofanyiwa watoto wetu katika jamii.” Alisema Mkuu wa Wilaya.

Aidha katika hatua nyingine alilipongeza shirika lisilo la kiserikali la Hoja project Tanzania kupitia kwa Mkurugenzi wake Oswin Mahundi kwa kushirikiana na Wilaya ya Nyasa kuandaa na kufadhili maadhimisho hayo na kutoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano wa kuandaa maadhimisho mengine yatakayo fanyika katika Wilaya ya Nyasa.

Aidha, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Nyasa, Bwana Douglas Ruambo, aliihamasisha jamii kuwatunza watoto na kuimarisha ulinzi wa watoto ili waweze kuwakomboa watoto kifikra kwa kuwa ni haki yao na pasipo kuwatunza watoto hatuwezi kuwa na jamii bora kwa kuwa watoto ni Taifa la kesho.

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa huadhimisha Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika kila mwaka Juni 16 na mwaka jana yaliadhimishwa katika Kijiji cha Tingi, wilayani hapa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.