• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MWAKA 2017 WILAYANI NYASA YAFANA.

Posted on: May 9th, 2017

Wilaya  ya Nyasa imepokea kwa shangwe,nderemo na vifijo Mwenge wa uhuru  2017,ambapo tarehe 07-05-2017 wananchi na Viongozi wa serikali kwa pamoja walikusanyika katika kijiji cha ukuli hususani katika viwanja vya shule ya msingi  ukuli katika kupokea mwenge huo na baadae kuelekea katika viwanja vya stendi ya mabasi wilayani nyasa.

Mwenge wa uhuru mwaka 2017 uliwasili viwanja vya shule ya msingi Ukuli majira ya saa (08;00) mbili kamili asubuhi ukiongozwa na kiongozi wa Mbio za mwenye mwaka huu Ndg Amour Hamad Amour na kupokelewa kwa furaha kabla ya makabiziano rasmi yaliyofanyika kati ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bw. Cosmas Nshenye na kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bw. Juma Homera.  

Baada ya makabiziano hayo, Shangwe zilizoambatana na Ngoma, mganda na kioda ziliendelea katika viwanja hivyo hata kupelekea wakimbiza mwenge kitaifa kupata hamasa kwa burudani hizo, Baada ya burudani hizo ulifuata utambulisho, Nasaha na Ujumbe wa Mwenge mambo yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, katika hatua hii Kaimu mkuu wa Wilaya alimweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka 2017 kwa kifupi Ratiba ya mwenge huo kwa siku nzima na itafanya shughuli zipi kwa manufaa ya wananchi, kisha ukafika wakati wa Mbunge wa Nyasa Mh. Eng Stella Manyanya kuwasalimia Wananchi , ambapo katika maneno yake aliwaeleza Wakimbiza Mwenge na viongozi wengine kuwa wananchi wa Nyasa wanaupokea mwenge wa uhuru kwa furaha na pia wanauheshimu na kuuthamini hasa kutokana na faida zake hivyo aliwakaribisha wakimbiza mwenge wote Wilayani nyasa na kuwaahidi ushirikiano wa kutosha kutoka kwake yeye na wapigakula wake.

Ulipofika wakati wa kutoa ujumbe wa mwenge ndg. Amour Hamadi alimshukuru Mh. Naibu Waziri wa Elimu na Mbunge wa Nyasa kwa uzalendo wake na hatimaye kuweza kuwepo mahala pale kwa mapokezi ya mwenge wa uhuru jambo ambalo huko walikotoka awakuliona na kisha kumwomba awafikishie salamu zao kwa Viongozi huko Bungeni (Spika) na kwamba wanaendelea vyema, pamoja na pongezi hizo ulitolewa ujumbe wa mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017.

Katika hotuba yake, Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2017 aliwaeleza wananchi wa nyasa kuwa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 umebeba ujumbe maalum mkubwa mmoja na Kauli mbiu  zake zipatazo nne, ambazo ni pamoja na

“SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU” wenye Kauli Mbiu zifuatazo:

  • “MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, TUWAJALI NA TUWASIKILIZE WATOTO NA VIJANA.
  • “TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI INAWEZEKANA IFIKAPO MWAKA 2030”
  • “TUUNGANE KWA PAMOJA DHIDI YA RUSHWA KWA MAENDELEO, AMANI NA USALAMA WA TAIFA LETU”
  • “SHIRIKI KUTOKOMEZA MALARIA KABISA KWA MANUFAA YA JAMII”

Baada ya kukamilika kwa kazi ya kutoa ujumbe wa mwenge wa uhuru safari ya kutembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo ilianza ambapo miradi iyo aidha ilizinduliwa ,kuwekewa mawe ya msingi, kukaguliwa au kutembelewa hatua kwa hatua kama ifuatavyo

  1. Kutembelea Mtambo wa kumenyea kahawa wa chama cha nambawala kijiji cha ukuli
  2. Kuweka jiwe la msingi Chama cha akiba na mikopo kingerikiti
  3. Kukagua Mradi wa shamba la kahawa
  4. Kuzindua mradi wa upandaji miti kibiashara
  5. Kuweka jiwe la msingi mradi wa maji wa litindoasili-lumecha
  6. Uzinduzi wa kituo cha redio ya Jamii Nyasa (Unyanja FM)
  7. Kuweka jiewe la Msingi kwenye barabara za mitaa kilometa nane.
  8. Kutembelea mradi wa ufyatuaji matofali kwa tekinologia rahisi.
  9. Uzinduzi wa mradi wa ufugaji kuku kibiashara
  10. Ufunguzi wa jengo la upasuaji na wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha mbamba bay
  11. Kuweka jiwe la msingi vibanda vya wajasilia mali-mbambabay
  12. Uzinduzi wa boti la doria ya uvuvi haramu na uokoaji  kituo cha usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi mbamba bay
  13. Kuweka jiwe la msingi vyumba nane vya madarasa katika shule ya sekondari mbamba bay
  14. Uzinduzi wa soko kuu la kilosa

 Baada ya ziara hiyo katika miradi mbalimbali, mwene wa uhuru ulielekea viwanja vya mkesha ambapo mambo yafuatayo yalifanyika:

  • Kugawa fedha  kwa wajasiliamali wa  soko la kilosa
  • Pia risara ya utii kwa Mh Rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ilisomwa .
  • Aidha wananchi wa Nyasa walipokea mwenge wa uhuru na kuunga mkono kauli mbiu za Mwenge kwa kujitokeza kwa wingi  kupima VVU na  maralia ili kupambana na magonjwa hayo.

  Baada ya matukio hayo mamia ya wakazi wa nyasa  wakiwemo wazee walijitoa  usiku kucha katika kusherekea    Mwenge wa uhuru wilayani Nyasa ,ambapo ngoma na burudani mbalimbali ziliendelea kulindima  hali iliyoonesha uzarendo, umoja na ushirikiano wa hali ya Juu kwa wananchi wanyasa.

Baada ya shamrashamra za Mkesha wa usiku kucha Mwenge wa uhuru ulipelekwa katika kijiji cha Buruma kwa ajili ya makabidhiano  ambapo kaimu Mkuu wa Wilaya Bw Juma Omera alikabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga .

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.