• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MAENDELEO YA MRADI WA PANDA MITI KIBIASHARA NYASA WARIDHISHA

Posted on: July 9th, 2020

Mradi wa Pandamiti kibiashara unaotekelezwa katika safu ya Milima ya Livingstone, katika Kata za Lipingo, Liuli, na Kihagara katika Wilaya ya Nyasa unaendelea kwa kiwango cha kuridhisha licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Mradi wa Forvac Mkoa wa Ruvuma Bw.Marcel Mtunda, hivi karibuni  Wakati akikagua mradi wa panda miti kibiashara unaotekelezwa  katika kijiji cha Mkali A na Kijiji cha Nkalachi Kata ya Liuli Wilayani hapa.

Bw alifafanua kuwa ameridhishwa na maendeleo ya ukuaji wa miti, na kuwaomba wananchi wapalilie miti hiyo, ili isiungue na moto, na amefurahi kuona  wananchi mara baada ya kupata elimu ya upandaji miti kibiashara, walivyohamasika na kupanda miti Hekari 317.5 , hali iliyompa ari ya kuongeza  miche ya miti ambayo kwa mwaka jana ilipungua.

Aliongeza kuwa , Mradi wa pandamiti kibiashara unaotekelezwa katika maeneo yao ni Mradi ambao utawanufaisha wakulima wa Miti katika vijiji hivyo kwa kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato katika ngazi ya Familia na Halmashuri kwa ujumla kwa kuwa miti aina ya Mitiki ni Miti inayostawi katika ukanda huu na Serikali inataka kuinua Maisha ya Wnanchi wa Wilaya ya Nyasa.

Alitoa Wito kwa Wananchi Wiayani Hapa kuchangmkia Fursa ya Upandaji miti kibiashaa ambao unatekelezwa katika maeneo yao kwa kuwa ni mradi unaowahusu wananchi wa Nyasa ambao wanapewa ardhi ya upandaji miti,miche ya Mbegu na huduma za elimu ya upandaji miti Kibiashara.

‘’Kwa kweli nimeridhishwa na upandaji miti Kibiashara mradi unaotekelezwa na Mradi wa Forvarc katika Kata hizi za Lipingo,liuli, na Kihagara kwa kweli unaendelea vizuri miti imeota vizuri na inaaliliwa kwa wakati kiasi kwamba hata wafadhili wakiona wanafurahia maendeleo ya Mradi huu japo kwa saasa tunachowaomba wananchi watengeneze barabara za kukinga moto kwa kuwa msimu tunaoenda n wa moto hivyo tunaomba kila mwananchi ahakikishe shamba lake liwe safi kwa kuwa moto ukiunguza miti  mradi utakuwa hatiani’’.

Alizitaja changamoto zinazo ukabili mradi ni ukosefu wa miundombinu ya Barabara na Madaraja, katika Mto Mbawa na mito mingine, ambayo husababisha wakulima kutokwenda mashambani wakati wa masika kwa kuwa maji hujaa katika Mito, na kuhamisha madaraja ya muda yaliyojengwa na wananchi.

Aliitaja changamoto nyingine kuwa, ni mgogoro wa meneo kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbinga na Nyasa hali inayowafanya wananchi wa Wilaya ya Mbinga Kuharibu miti japokuwa ,viongozi wakuu wa Wilaya wameshamaliza mgogoro huu na kuendelea vizuri kwa ukuaji wa Miti hiyo.

Ofisa Maliasili wa Wilaya ya Nyasa Bugingo Bugingo alisema Halmashauri ya Nyasa imeweka lengo la Kupanda miti ekari  1750  na mpaka sasa miti ekari 317.5imepandwa na inaendelea vizurisana na kuwataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa wachangamkie fursa ya upandaji miti Kibiashara kwa kuwa na Mradi muhimu utakaowanufaisha hapo baadae.

“Ndugu wananchi Mradi huu utawanufaisha wenyewe kwa kuwa baadhi ya wananchi wanawapotosha kuwa miaka 18 hadi 20 ni muda mrefu sana hutaweza kuvu a lakini angalia ukika tuu utapata faida gani? wakati ukipanda hii miti baada ya miaka 20 unataraia kupata zaidi ya Miliono 400,  kwa ekari moja. Ndugu zangu tunatakiwa kupanda miti kwa hali na mali kwa kuwa mbegu tunapewa bure, Ardhi inapatikana bure  hivyo tunatakiwa kuongeza juhudi ili kufikia malengo ya kupanda ekari 1750 kwa Wiaya ya Nyasa” Alisema Bugingo.

Aliongeza pia katika misitu hiyo pia tuntarajia kuanzisha ufugaji wa Nyuki ili tuweze kuvuna asali nayi itatusaidia kuingiza kipato cha familia na Halmashauri kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wiaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama alisema Wiaya ya Nyasa,  tunaeneo kubwa la upandaji miti aina zote inayostawi katika ukanda wa ziwa yaani maeneo yenye joto, na Ukanda wa milimani yaani maeneo yenye baridi kama vile Tarafa ya Mpepo ambayo ardhi yake inastawisha sana Miti ambayo hustwi maeneo yenye Baridi.

Hivyo ametoa Wito kwa wananchi, makampuni na wawekezaji wanaohitaji kuwekeza sekta y a Misitu  Wilayani Nyasa kuwekeza ili wilaya iweze kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwa halmashauri zingine zilishaanza kuwekeza katika Sekta ya Upandaji miti na wamekuwa wakijipatia manufaa mbalimbali ikwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo na Kuongeza kipato katka Ngazi ya Familia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Isabela Chilumba aliwapongeza sana wananchi kwa kuchangamkia Fursa ya Kupanda miti Kibiashara, na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano  Tanzania kwa kuleta Mradi wa Forvarc katika Halmashauri ya Nyasa na kuwaomba Wananchi wapande miti na kuwakikishia Serikali itatatua changamoto zote zinazo wakabili wananchi hao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za Kisheria wale wote wanaohusika kuharibu au kufifisha maendeleo ya Mradi huu wa Pandamiti Kibiashara

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.