• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MAAJABU YA FUKWE ZA MHALO ZIWA NYASA UNAWEZA KUONA MIPAKA YA NCHI MBILI KWA WAKATI MMOJA

Posted on: October 16th, 2020

Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imebarikiwa kuwa na fukwe za asili katika ziwa Nyasa ambazo hazifanani na fukwe nyingine zozote duniani na endapo zitaendelezwa zinaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato kwa serikali na wananchi.

Fukwe ya Mhalo iliyopo katika kijiji cha Ruhekei Kata ya Kilosa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa  imeendelezwa kwa kujengwa vivutio vya utalii pamoja na hoteli ya Mhalo beach Lodge iliyojengwa mwambao mwa fukwe za Mhalo.

Benado Lisambo ni Meneja wa Mhalo Beach Lodge  anasema fukwe hizo zina maajabu ambayo hayawezi kupatikana sehemu nyingine hali ambayo inavutia wageni wengi wa ndani na nje ya nchi kufanya utalii na kupata huduma zote zinazostahili kwa watalii.

Anakitaja kivutio kikubwa katika fukwe hizo kuwa ni mtalii anaweza kuona mipaka miwili ya nchi mbili  za Malawi na Msumbiji kwa wakati mmoja jambo ambalo linawavutia watalii wengi wanaotembelea fukwe hizo.

“Sisi wilaya Nyasa tuna bahati sana,ukiwa hapa Mhalo beach ukiangalia kusini unaona milima ya nchi ya Msumbiji na ukiangalia Magharibi unaona milima ya nchi ya Malawi,wakati wa usiku unaweza kuona taa za magari katika nchi hizo kwa kweli inavutia sana’’,anasisitiza Lisambo.

Hata hivyo anasema fukwe yote ya Mhalo inavutia wageni wengi wa ndani na nje ya nchi kwa sababu haina uchafu,maji yake ni maangavu hali ambayo inamwezesha mtalii kuwaona samaki  wanavyotembea ndani ya maji katika ziwa Nyasa.

Kulingana na Meneja huyo,toka fukwe ya Mhalo hadi mpakani na nchi ya Msumbiji ni umbali wa kilometa 30 na kwamba unaweza kusafiri kwa boti kupitia ziwa Nyasa na kwamba  kusafiri kwa boti toka fukwe ya Mhalo hadi nchini Malawi ni safari ya saa sita.

Anawataja watalii ambao wametembelea fukwe za Mhalo kuwa wametoka nchi za  Ujerumani, Italia, Uingereza, Marekani, Japan,Afrika ya Kusini,Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na kwamba wanapokea pia watalii wengi kutoka ndani ya nchi.

“Watalii wakifika hapa Mhalo beach kuna vivutio vingi,   wanaweza kufanya utalii wa kuogelea,kupanda milima ya Livingstone, kutembea ufukweni kilometa mbili,kuona ngoma za asili mwambao mwa ziwa Nyasa,ikiwemo ngoma ya mganda,kioda na lindeku na kufanya safari za majini kwa kutumia boti’’,anasema Lisambo.

Joseph Ndomondo Mwongoza watalii Mkazi wa Liuli ziwa Nyasa anasema fukwe za ziwa Nyasa upande wa Tanzania ni bora zaidi kwa kuwa ni za asili ambazo zimetengenezwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe.

“Fukwe za ziwa Nyasa upande wa Malawi zimetengenezwa toka kingo za milima hivyo zimechimbwa hali ambayo inadhihirisha ubora wake hauwezi kulingana na fukwe za ziwa Nyasa upande wa Tanzania’’,anasema Ndomondo.

Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bugingo Bugingo anasema ziwa hilo limebarikiwa kuwa na fukwe nzuri za asili na zinazofaa kwa uwekezaji kwenye sekta ya utalii hivyo ametoa rai kwa wawekezaji kuwekeza ziwa Nyasa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.