• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KAMPUNI YA GODMWANGA YATOA MIFUKO 70 YA SARUJI KIJIJI CHA MALINI

Posted on: June 15th, 2020

Kampuni ya Godmwanga inayochimba makaa ya mawe katika Kijiji cha Malini Kata ya Mtipwili Wilayani Nyasa, imetoa saruji mifuko 70,yenye thamani ya tsh milioni moja (1,000,000/=) kwa ajili ya kuchangia miradi mitatu ya afya na  elimu Kijijini hapo.

Saruji hiyo imekabidhiwa jana, katika viwanja vya ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Malini, na mwakilishi wa Mkurugenzi wa  kampuni ya Godmwanga, Bwana Alen Kimaro na kupokelewa na Wananchi wa kijiji hicho huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba.

Akikabidhi Saruji hiyo, katika Mkutano wa Hadhara, bw kimaro alisema kuwa, kampuni inayochimba makaa ya mawe katika kijiji hicho kimethamini shughuli mbalimbali za maendeleo, zinazofanywa na wananchi pamoja na Serikali katika Kijiji hicho na Kampuni imejiridhisha , na kuwataka wananchi kuhakikisha saruji hiyo inatumika kama ilivyokusudiwa .

Aliongeza kuwa, saruji  ameitoa kwa mchanganuo, mifuko (50) ni kwa ajili ya Ukarabati wa Darasa la awali la shule ya Msingi Malini, Mifuko kumi ni kwa ajili ya Ukarabati wa Zahanati ya Chiulu na mifuko 10 kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtipwili.

“Ndugu zangu Kampuni ya Godmwanga leo imeona itatue changamoto ya mifuko 70 ya saruji kama mlivyoomba, kwa kuwa sisi tunafanya kazi katika maeneo yenu kama mlivyotukaribisha  na ni wamoja na tunathamini shughuli za kimaendeleo mnazofanya, hasa za Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya elimu na afya leo tumeona tuanze na mifuko 70 ya saruji na tutaendelea kuwaunga mkono kadiri mtakavoona inafaa” alisema kimaro

Alitoa wito kwa wananchi na makampuni mengine kuiunga mkono Serikali ya awamu ya Tano kwa kuchangia Miradi ya maendeleo ili kuboresha Huduma kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba aliipongeza kampuni hiyo, kwa kuchangia kiasi hicho cha saruji kwa kuwa msaada huo umetatua kero ya wananchi wa Kijij cha Malini na kuwaomba, waongeze juhudi za kushirikiana na Serikali pamoja na wawekezaji ili kujiletea maendeleo.Aidha alichangia tsh (300,000)ili kuunga mkono juhudi za maendeleo kijijini hapo.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Yohana Ndunguru kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho aliishukuru kampuni ya Godmwanga, kwa kutatua changamoto hiyo ya saruji  na kusema ni kweli walikuwa wanauhitaji wa saruji hiyo na atahakikisha inatumika vizuri.

Kampuni ya Godmwanga inachimba makaa ya mawe katika Kijiji cha Malini Kata ya Mtipwili Wilayani hapa  na kuuza sehemu mbalimba za nchi kama vile Kiwanda cha Dangote,Mbeya Cement na sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Announcements

  • Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyasa December 01, 2025
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Balozi wa Tanzania nchini Malawi atembelea Wilaya ya Nyasa

    December 06, 2025
  • Maonesho ya Nane Nane Kanda za Nyanda za juu kusini , Mguu sawa Kuanza leo

    August 01, 2025
  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.