• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KITUO CHA RADIO JAMII (UNYANJA FM) CHAZINDULIWA

Posted on: May 8th, 2017

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017 Bw. Amour Hamad Amour Tarehe 07-05-2017 amefanya uzinduzi rasmi wa Radio Unyanja FM na kuanza kurusha matangazo yake kutokea majengo ya Parokia ya Nangombo iliyopo katika kata ya Kilosa, Awali kituo hicho kilikuwa kikirusha matangazo yake kwa majaribio kuanzia Julay 2016

Mwenge wa uhuru umefanya uzinduzi huo ukiwa ziarani wilayani  nyasa baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo huko katika kijiji cha Ukuli kata ya Kingerikiti kabla ya kusafiri zaidi ya Kilomita 41.1 na kufika hapa kijiji cha Nangombo.

 

Baada ya kuwasili katika eneo la uzinduzi kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017 alisomewa taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa kituo cha kurushia  matangazo cha muda na namna taratibu zote za usajiri zilivyofanyika na kukamilika. Taarifa hiyo ilisomwa na msimamizi mkuu wa kituo Bw.Patrick Kosima

Katika taarifa yake, Msimamizi wa Kituo alimweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mwaka 2017 kuwa Mwaka 2014 hadi 2017 shirika lisilokuwa la Kiserikali Agriculture and Micro-enterprise Development Organization (AGROMICRODET) kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa walianza kutekeleza Mradi wa kuanzisha Redio ya Jamii chini ya ufadhili wa shirika la Programu za maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambapo malengo yao ni kusikika katika maeneo ya mkoa wa Ruvuma yote japo mpaka sasa usikivu wake ni wa kiwango kizuri katika maeneo ya  Mwambao mwa ziwa Nyasa pekee, lakini jitihada zinafanywa kufikia lengo husika

 

Aidha lengo la kuanzishwa kwa Redio Unyanja ilikuwa ni kukidhi hitaji la wilaya ya Nyasa na Mwambao  wa ziwa la kuwa na Redio inayotangaza kwa Kiswahili kwa kuwa akukuwa na matangazo yoyote yaliyokuwa yakisikika kwa lugha ya Kiswahili katika maeneo ya ziwa Nyasa na hivyo wananchi kukosa fursa ya kuhabarishwa na Kueleimishwa katika nyanja ya Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa hususani mpango wa Serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa Viwanda.

Pia katika taarifa yake alimwambia kiongozi wa Mbio za mwene wa uuru kitaifa mwaka 2017 kwamba Mpaka sasa Mradi umegharimu jumla ya fedha za kitanzania 155,000,000.00 kutoka katika vyanzo vifuatavyo -; Mchango toka kwa taasisi husika Tsh.17,500,000.00, Mchango wa Halmashauri Tsh.10,000,000 na Mchango toka kwa Wafadhili (UNDP) Tsh 127,500,000.00  ambapo fedha hizi zimetumika kwa kufanya shughuli kama Ukarabati wa majengo, Ununuzi wa vifaa vya redio, Usimikaji wa mitambo, Upatikanaji wa vibali na gharama za uendeshaji,  Aidha ujenzi wa jengo la kudumu la kurushia matangazo unatarajia kuanza huko kijiji cha kilosa.

Akizungumza na wananchi waliokusanyika katika eneo la uzinduzi na wale waliosikiliza redio Unyanja kwa wakati huo, Bw Amour hamad Amour aliitaka jamii ya Nyasa kuitumia radio Unyanja kama ngazi ya kupata habari na matukio yanayoendelea duniani kote na pia aliwaasa watangazaji na wasimamizi wa kituo hicho kuhakikisha wanarusha matangazo yale yenye maadili mema kwa taifa letu lakini pia kuwapatia wananchi habari zile zinazolenga kuwahakikishia kwenda sambamba na mawazo ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha na kuimarisha uchumi na hatimaye kufikia uchumi wa viwanda

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.