• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KAMPUNI YA SIGARA, YATATUA KERO KUBWA YA WALEMAVU NYASA

Posted on: December 15th, 2020

Kampuni ya Sigara Tanzania imekabidhi kwa Wilaya ya Nyasa,  vifaa vyenye thamani ya shilingi 14,367,500 kwa ajili ya walemavu wa  wilaya ya Nyasa.Vifaa vimekabidhiwa jana, katika hafla fupi iliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akikabidhi Vifaa hivyo Afisa Miradi wa Kampuni ya Sigara Tanzania Bw Oscar  Luoga, amesema kampuni ya Sigara imeona itoe Vifaa hivyo, kwa walemavu wa Wilaya ya Nyasa, ili kuwakwamua kiuchumi kwa kuwa shirika la Sigara linaamini katika kusaidia jamii, hasa yenye uhitaji,na kuunga juhudi za Serikali katika kuleta Maendeleo.

Amevitaja vifaa alikabidhi kuwa ni Baiskeli za Miguu mitatu 23, magongo 100, na Fimbo nyeupe 5 ambavyo viliombwa katika Kampuni yake na Mbunge wa Wilaya ya Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, kwa ajili ya kutoa Huduma kwa walemavu ili kuwasaidia waweze kutembea na kujikwamua katika shughuli mbalimbali zakiuchumi.

“Ndugu viongozi wa Wilaya ya Nyasa na wananchi wa Wilaya ya Nyasa kampuni ya Sigara Tanzania imeamua itoe vifaa hivi kwa ajili ya walemavu kwa kuwa tunaamini katika kusaidia wahitaji hasa  jamii yenye uhitaji na kwa mwaka huu tumeamua kuisaidia jamii ya wenye ulemavu Wilaya ya Nyasa hasa kwa kauli Mbiu inayotumika katika kampuni ambayo ni Tunaleta mabadiliko pamoja na, kutoa ni moyo”

Akizungumza katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, amewashukuru kampuni ya Sigara kwa kutoa vifaa hivyo kwa walemavu, ambao wamekuwa na uhitaji wa muda mrefu.kabla ya vifaa hivyo walemavu hao walikuwa wakitambaa chini, na wengine kutembea kwa shida kutokana na ukosefu wa Viungo mbalimbali vya mwili.

Aidha mbunge Manyanya alitoa shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwapa walemavu waliokusanyika, katika hafla hiyo kwa ajili ya kuanzisha biashara ndogondogo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Serikali Wilayani Nyasa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba, amewashukuru kampuni ya Sigara Tanzania kwa kuwakumbuka Walemavu wa Wilaya ya Nyasa na ameomba makampuni mengine yaweze kuunga mkono na kuwasaidia makundi mbalimbali ukizingatia Wilaya ya Nyasa iko mbali kutoka makao makuu ya Nchi.

“Nichukue fursa hii, kuwashukuru kampuni ya Sigara Tanzania kwa kuwatatulia changamoto walemavu wa wilaya ya Nyasa, niseme tu wako wengi lakini kwa sasa tunashukuru kwa hawa waliopata na tunazidi kutoa wito kwa Makampuni mengine waweze kuisaidia Wilaya ya Nyasa kwa watu wenye ulemavu, ukizingatia tuko mbali na makao ya Nchi Dodoma.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha watu wenye Ulemavu Bw. Bonifasi Mputa amesema anaipongeza Serikali, Kampuni ya Sigara na Mbunge wa Nyasa kwa msaada huo kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa watu wenye Ulemavu Wilaya ya Nyasa kupokea msaada huo.

Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Maafisa habari/Tehama wapewa Mafunzo Ruvuma

    May 29, 2023
  • Dc-Nyasa TASAF NI Kiboko Cha utatuzi Kero za wananchi

    May 23, 2023
  • Uvuvi haramu marufuku ziwa Nyasa, wenye Nyavu haramu wajisalimishe

    May 18, 2023
  • Kikao Cha kamati ya Lishe

    May 17, 2023
  • View All

Video

NYASA yampongeza Rais SAMIA jengo jipya la Utawala
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.