• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KAMATI YA SIASA MKOA WA RUVUMA YARIDHISHWA NA MRADI WA BWALO NYASA

Posted on: June 30th, 2020

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, imetoa Sh milioni 150 kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa bwalo na jiko, katika shule ya Sekondari ya Kilumba, Kata ya Lumeme Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashari ya Nyasa Oscar Elias amesema,  ujenzi wa Mradi huo umetekelezwa kwa kutumia Force account, ambao ulianza Septemba 20, 2019 na kukamilika Desemba 20 ,2019.

“Mradi umetoa ajira za muda kwa watu 60, ikiwa ni wanawake 16 na wanaume 44. Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa na wananchi wa Kata ya Lumeme, tunaishukuru Serikali ya CCM kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi’’,alisema.

Akizungumza baada ya kukagua Mradi huo, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Nuru Ngeleja, amesema Kamati ya Siasa ya CCM mkoa, imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

 Ngeleja amewaomba wananchi siku ya uchaguzi Mkuu  kujitokeza kwa wingi na kuwapigia kura Viongozi wa CCM, Kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani ili kuwatia moyo ya kuendelea kuwatumikia, katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake  (UWT) wa Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu Mhagama, amewapongeza wananchi wa Kata ya Lumeme, kwa kujenga bwalo, na bweni la Watoto wa kike katika Shule ya Sekondari Kilumba,ambapo amesema bweni litasaidia kupunguza mimba za utotoni.

Mhagama ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa  ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni, Hivyo amewaasa wazazi na walezi, kuwathibiti watoto wao ili kupunguza tatizo hilo na kuwawezesha watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM  Taifa, Musa Homera amesema ili kuonesha Shukrani  kwa, Rais John Magufuli,ameshauri kujitokeza kupiga kura nyingi za Ndiyo katika uchaguzi mkuu  Oktoba mwaka huu.

“Mimi nataka niwaambieni Shule, Hospitali na Majengo mengine ya Serikali yaliyojengwa Miaka 40 iliyopita, yanalingana na majengo yaliyojengwa kwa fedha za Serikali katika kipindi cha miaka mitano,  cha uongozi wa Rais Magufuli”, amesisitiza Homera.

Sera ya Elimu ya mwaka 2014 pamoja na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, inaipa kipaumbele sekta ya elimu na itahakikisha Serikali inasimamia sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014.

Imeandaliwa na 

Albano Midelo na Netho Credo

Maafisa Habari Serikalini

Mbambabay

Juni 29,2020

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • Wilaya ya Nyasa yaadhimisha miaka 61 ya Muungano kwa Kufanya Usafi

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.