• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KAMATI ya Siasa (CCM) Mkoa wa Ruvuma yampongeza Rais Samia Ukamilishaji daraja Mto Ruhuhu

Posted on: November 5th, 2021

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Ruvuma  leo Wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga na kukamilisha daraja la Mto Ruhuhu linalounganisha Mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia Wilaya ya Nyasa na Ludewa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Mh Oddo Mwisho ameyasema hayo kwa niaba ya Kamati nzima ya Chama hicho mara baada ya kutembelea daraja hilo na kukagua Miradi ya Maendeleo  ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama.

Amefafanua kuwa kwa miaka mingi daraja hilo lilikuwa kero kwa wananchi wa Ludewa na Nyasa, hasa katika shughuli mbalimbali na kama chama chao walipewa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwa kuwa mara nyingi wanachi walikuwa wakiliwa na mamba wakati wakivuka mto huo kutafuta huduma za kijamii kama za afya na nyinginezo, lakini leo wanampongeza Mh Rais Samia Suluhu Hasassan  kwa kukamilisha Ujenzi wa daraja hilo ambalo limefikia asilimia 99 na linapitika.

Ametoa Wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa na Ludewa kuitunza miundom binu iliyowekwa kwenye daraja hilo ili lidumu kwa miaka mingi zaidi na asitokee mwananchi yeyote kuiba, au kuharbu miundombinu ili daraja hilo litoe huduma kwa vizazi vijavyo huku wakikumbuka shida walizopata.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa daraja hili kunachochea shughuli za kiuchumi na Utalii kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa na Ludewa, kwa kuwa lilikuwa ni kikwazo cha wananchi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.

Miradi mingine ilkiyotembelewa ni Bandari ya Ndumbi ambayo imefikia asilimia 88 na mwezi Desemba mwaka huu inatarajiwa kukamilika na itakuwa inasafirisha makaa yam awe kutoka Wilayani Nyasa kuelekea sehemu mbalimbaki za ndani na nje ya Nchi kamati hiyo pia imeridhishwa na ujenzi wa bandari hiyo.

Mradi wa Mwisho ni Bustani ya Kitalu cha miti ambacho  kuna miche laki saba ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo ya Serikali na kuwagawia wananchi bure ili kuwahamasisha kupanda miti ya mitiki katika maeneo yao ili kuunga juhudi za Serikali za kuhamasisha upandaji miti ya mItiki Wilayani Nyasa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.