• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa atambulisha Mradi wa Maji Tingi malungu,kuhudimia wakazi 9659

Posted on: December 6th, 2022

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya  Nyasa mh.Aziza mangosongo  Tarehe 05/12/2022 amefanya Ziara ya kikazi ya Siku moja Wilayani Nyasa, na kufanya shughuli mbalimbali  katika Kata ya Kilosa, na Tingi.

Katika Kata ya Kilosa ameshiriki Upandaji miti katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa ili kuadhimisha  miaka 61 ya  Uhuru wa Tanzania Bara, na katika Kata ya Tingi amefunga mafunzo ya Mgambo, na kumtambulisha mkandarasi anayetekeleza Mradi wa maji wa Tingi Malungu.

Akiwa katika Kata ya Kilosa amewataka wananchi, kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji ili kuenzi Uhuru wa Tanzania bara, na kulinda amani iliyopo katika Nchi yetu ya Tanzania. Amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuhamasika na kushiriki shughuli za usafi na upandaji miti katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa na kutoa wito kwa wananchi hao kuendelea kupanda miti katika maeneo yao, ili kulinda na kuhifadhi mazingira na Vyanzo vya maji.

Katika Kata ya Tingi amefunga mafunzo ya jeshi la akiba ambao jumla ya wahitimu 89 wamehitimu mafunzo hayo na kuwataka kutumia mafunzo waliyopewa kwa kuwa wazalendo na kuitumikia nchi yao katika shughuli za uzalishaji mali.

Amewapongeza wahitimu hao kwa kufyatua tofari 15000 (elfu kumi na tano ) kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika shule ya Sekondari ya Tingi.

Katika Kijiji cha Malungu kata ya Tingi amemtambulisha Mkandarasi PEACE CONSTRUCTION LMTD katika mkutano wa hadhara, ambaye anajenga mradi wa maji wa Tingi Malungu utakaohudumia vijiji 2 vya Tingi na Malungu amabao unatarajia kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi 9659 mradi wenye gharama ya  Tsh 487,530,225.

Mradi huu utatekelezwa kwa muda wa miezi sita na  kazi zitakazofanyika ni ujenz wa Tank lenye Lita Laki moja  na vituo vya kuchotea maji 11 pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji.

Mh Mangosongo amemuagiza mkandarasi kufanya kazi kwa bidii na kukamilisha mradi kwa muda uliopangwa, na kuwataka wananchi kushirikiana na Mkandarasi huyo ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri.

Ametoa wito kwa wananchi kutnza miundombinu  na vyanzo vya maji ili kuwa na uhakika wa maji safi na salama kwa kuwa Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji safi na salama kwa wakazi wa vjiji hivyo.

Kwa upande wao wananchi wameipongeza Serikali kwa kutatu kero ya maji katika vijiji hivyo kwa kuwa walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji. Aidha wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh, Aziza Mangosongo kwa kufanya zira za mara kwa mara wilayani hapa na kukagua miradi ya maendeleo.

Imeandaliwa na Netho C. Sichali

Afisa Habari ,Kitengo cha Mawasiliano,

Wilaya ya Nyasa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.