• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

JIWE LA POMONDA LIULI LINA VIVUTIO VYA KILA AINA

Posted on: January 21st, 2021



KAMA unadhani jiwe la Mwanza lililopo katika ziwa Viktoria ndiyo kivutio pekee cha utalii katika maziwa hapa nchini utakuwa unajidanganya.

Katika ziwa Nyasa Mkoa wa Ruvuma kuna jiwe linaloitwa Pomonda ambalo linavivutio lukuki vya utalii ambavyo vinavutia wengi waliobahatika kufika katika jiwe hilo.Jiwe la Pomonda lenye ukubwa wa robo hekari ambalo lipo meta takribani 300 ndani ya ziwa Nyasa  kutoka bandari ya Liuli.

Muongozaji watalii katika bandari ya Liuli Joseph Ndomondo ambaye pia ni Mmiliki wa fukwe ya Pomonda anasema Jiwe la Pomonda ambalo wajerumani walilipa jina la sphinxhaven kutokana na kuwa na vivutio lukuki.

Utalii wa kihistoria ni aina ya kwanza ya utalii ambayo inapatikana katika jiwe hilo ambapo tangu vita ya kwanza ya dunia mwaka 1914 hadi 1918  na vita ya pili ya dunia mwaka 1939 hadi 1945  wakoloni walitumia jiwe hilo kujificha.

Anasema wajerumani na waingereza walitumia pango kubwa lililopo katika jiwe la Pomonda ambalo lipo kama ukumbi wenye kubeba watu kati ya 60 hadi 100 hivyo wanajeshi  wa kiingereza na kijerumani walitumia jiwe hilo kama sehemu ya kujificha wakati wa  mapambano.

Katika jiwe hilo inaaminika kuna sahihi ya Dk.David Livingstone Mvumbuzi maarufu ambaye alivumbua milima Livingstone ambayo pia imepewa jina lake kuzunguka ziwa Nyasa.

Dk.Livingstone alizaliwa huko Blantyre,Uingereza Machi 19 mwaka 1813.Alisoma masomo ya udaktari wa binadamu katika Chuo Kikuu cha Cambridge.Alifanya safari za kuja Afrika mara tatu kwa nyakati tofauti.

Ilikuwa ni mwaka 1866 ambapo Dr. Livingstone alikuja Afrika kwa mara ya tatu.Lengo la safari yake lilikuwa ni kuchunguza chanzo cha mto Nile.Safari yake ilianzia katika chanzo cha mto Ruvuma, Mikindani Mtwara hadi ziwa Nyasa, Banguela na Mweru.

Uchunguzi ambao umefanywa katika Jiwe la Pomonda umebaini kuwa kilele cha jiwe hilo ambacho kina urefu wa takribani meta 40 kwenda juu ipo taa maalum  kubwa yenye rangi nyekundu ambayo ilikuwa itatumiwa  na nchi tatu za Tanzania,Malawi na Msumbuji.

Taa hiyo ilitumika wakati wa wakoloni wa kijerumani,kireno na waingereza kwa ajili ya alama ya kuongozea meli katika ziwa Nyasa ili wasiweze kupotea  wanapotaka kutia nanga kwenye bandari ya Liuli,taa hiyo iliwawezesha kuiona bandari ya Liuli  hata wakiwa katika nchi za Malawi na Msumbiji.

Kivutio kingine cha utalii ambacho kinapatikana katika eneo la jiwe hilo ni mawe matatu makubwa ambayo wakazi wa eneo hilo wanaamini yamepangwa na Mwenyezi Mungu ,huku mpangilio wake ukiwa ni kivutio cha ajabu utadhani yamejengwa na mafundi ujenzi huku yakiwa yameacha njia maalum ambayo unaweza kupita kwa mtumbwi au boti kutokea upande wa pili hali ambayo inawashangaza na kuwavutia wengi.

Jiwe la Pomonda pia ni sehemu muhimu ambayo inafaa kufanya utalii wa michezo ya kwenye maji(water sports) kwa mfano mchezo wa kupiga mbizi  na  kuruka toka juu ya jiwe la Pomonda hadi ziwani umbali  wa karibu mita 30.






Matangazo

  • TANGAZO la vigezo vya kupata leseni ya biasharaJuly 31, 2021
  • TANGAZO la fursa za uwekezaji mkoani RuvumaMay 31, 2021
  • ILANI ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020/2025May 31, 2021
  • Tazama zote



Habari Mpya

  • JIWE la Pomonda ziwa Nyasa lina vivutio vya kila aina

    January 21, 2021


  •  
  • KISIWA maarufu cha Lundo kinachofaa kuwekeza katika sekta ya Utalii

    January 20, 2021


  •  
  • MTO Ruvuma ulivyoubeba Mkoa wa Ruvuma

    January 20, 2021


  •  
  • RUWASA yatekeleza maagizo ya RC Mndeme,Madaba waanza kupata maji ya bomba

    January 19, 2021


  • Tazama zote




Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.