• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Je umewahi kuliona Likungu karibu 88 Mbeya

Posted on: August 3rd, 2024

Likungu kivutio,Ndani ya Viwanya vya John MwakangaleJijini Mbeya.

ZIWA Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na Msumbiji.Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari.

Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na jumuiya ya nchi zilizo kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na  nchi ya Uingereza kwenye ziwa Nyasa,ulionesha kuwa ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki.


Licha ya kuwa na samaki wa aina mbalimbali,ziwa Nyasa pia lina utajiri wa maliasili nyingine ambazo huwezi kuzipata mahali popote duniani.


Moja ya maliasili asili hizo adimu ambazo zinaweza kukuza uchumi wa watu wa Mwambao mwa ziwa Nyasa ni wadudu ambao wanafahamika kwa jina la likungu ambao wanapatikana kwenye ziwa hilo pekee.


Likungu ni kitoweo ambacho kinatajwa na wataalam wa afya kuwa na utajiri wa protini na madini mengi ya chuma kuliko vyakula vingine   hali ambayo inasababisha wananchi wanaokifahamu chakula hiki kukigombania kinapopatikana na kusababisha kuwa na soko kubwa kwa walaji.


Ukibahatika kuona  likungu  limendaliwa kuwa kitoweo huwezi kutambua kuwa hao ni wadudu mfano wa mbu ambao wametengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu badala yake unaweza kudhani ni aina fulani ya nyama au samaki wanaopatikana ziwa Nyasa.


Efonsia Turuka(50) Mkazi wa Kijiji cha Hongi Kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma anasema ameanza kula likungu tangu alipokuwa ana umri wa miaka saba na kwamba kitoweo hicho ni muhimu kiuchumi na kiafya.


“Likungu ni chakula cha asili cha watu wa mwambao mwa ziwa Nyasa kinapendwa na wengi kutokana na kuwa na virutubisho adimu pia kina ladha tamu na kusababisha wengi kupenda kula ingawa upatikanaji wake ni sio wa kila siku.’’, anasisitiza Turuka.


Turuka ni mwanamke ambaye anatengeneza wadudu hao na kuwa kitoweo anasema akinamama wengi mwambao mwa ziwa Nyasa wana ujuzi wa kutengeneza wadudu hao kuwa kitoweo ambacho kinaweza kutumika kwa muda mrefu.


James Chale mkazi wa Liuli anasema wadudu kabla ya kukamatwa nchi kavu na kutengenezwa kitoweo wanaanzia kuruka angani katikati ya ziwa Nyasa kwenye mpaka wa Tanzania na nchi ya Malawi hadi kufika ufukweni mwa ziwa na kutua kwenye miti.


Challe anasema, inaaminika wadudu hao wanaotengeneza likungu wanatoka chini ya ziwa Nyasa na kuibuka juu ya ziwa wakiwa ndani ya  mfano wa puto la asili.


“Wakishaibuka juu ya ziwa puto hilo hupasuka na wadudu hao kusambaa hewani kwa mbali wanaonekana mfano wa kimbunga  ambacho kinakwenda taratibu  kulingana na kasi ya upepo hadi nchi kavu.


Anasema wanawake wakiona hali hiyo wanajiandaa kuwakamata wadudu hao ambao baada ya kufika nchi kavu wanatua kwenye majani ya miti iliyopo jirani na ziwa Nyasa.


Veronika Kamanga mkazi wa Liuli  anasema wadudu hao wakitua kwenye majani ya miti akinamama wakiwa na vifaa maalum kama vile vikapu walivyovilowanisha kwa maji wanatumia mianzi  kufunga vikapu hivyo na kuanza kuwakusanya wadudu hao ambao wanajaa kwenye vikapu hivyo na baadaye kuwafinyanga na kuwatengeneza katika maumbo tofauti yakiwemo duara au ngumi.


“Mara baada ya likungu kutengenezwa katika umbo la duara akinamama wanazungushia majani ya migomba kisha wanatumia mkaa kuanza kulichoma hadi majani ya mgomba yanapokuwa yameungua yanaashiria kuwa likungu limeiva hivyo wanatoa kwenye mkaa tayari kwa kuliwa’’,anasema.


Hata hivyo anasema likungu hilo kabla ya kuliwa kama kitoweo wakazi wa mwambao  wanaunga kwa kutumia karanga,nazi  au kuchemsha kwa maji na chumvi.


Likingu ili liweze kusafirisha maeneo ya mbali kutoka ziwa Nyasa,akinamama hao  wanaendelea kulikausha kwenye jua ili lisiweze kuharibika na kwamba likungu linaweza kukaa bila kuharibika kwa siku 30.


Likungu mwambao mwa ziwa Nyasa linauzwa kati ya shilingi  2,000 kutegemeana na ukubwa wake.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.