• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Hospitali ya Wilaya ya Nyasa yazindua Huduma ya Kulaza Wagonjwa na Upasuaji.

Posted on: July 20th, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa,  leo imezindua rasmi na kuanza kutoa,  huduma za kulaza wagonjwa na Upasuaji wa Dharula, katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa iliyojengwa katika Kijiji cha Nangombo, Kata ya Kilosa Wilayani Hapa.

 Akizindua Huduma hizo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kanali Laban Thomas, amewata watumishi na wahudumu  wa Afya Wilayani hapa   kutoa huduma bora kwa Wazee, na wananchi na  wanaofika kupata huduma za matibabu katika Hospitali  ya Wilaya,  na kufanya kazi kwa bidii na  kufuata maadili ya kazi pamoja na viapo walivyokula.

Kanali laban amefafanua kuwa , mara baada ya kuanza kutoa huduma ya kulaza wagonjwa, na Upasuaji wa Dharula, ni mategemeo yake kuwa,  huduma  zitaboreshwa, na wananchi watapata huduma bora za afya, na Wazee watathaminiwa zaidi ili kuwaenzi, kwa kazi walizofanya kipindi wakiwa vijana za kulijenga Taifa la Tanzania.

Ameongeza kuwa atafurahi zaidi atakapoona Wazee wakipewa huduma bila kuwabagua, wala kuwasumbua, kwa kuwa nao wamechangia huduma nyingi za kulijenga Taifa letu, na kuwataka watumishi, kutoa Huduma kwa kufuata Sheria Taratibu na Kanuni kwa kuzingatia Viapo walipoapa.

“Ndugu wananchi wa Wilaya ya Nyasa na Watumishi wa Afya,  leo tukiwa tunafungua Huduma hizi za Kulaza wagonjwa, ninawataka, kuwapa Huduma bora wazee ambao nimewaalika leo, katika Zoezi hili  ili waone tunavyozindua huduma hizi, na ninawaagiza wazee hawa tunatakiwa kuwajali kwa kuwapa huduma bora, kwa kuwa nao walishafanya kazi za kulijenga Taifa .Aidha watumishi na Wahudumu wa Afya mnatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa na wateja kwa kuwa wagonjwa wanahitaji hata faraja kutoka kwa Mtoa Huduma za Afya”. Amesema Kanali Thomas.

Awali akisoma Taarifa ya Uzinduzi wa Huduma za kulaza wagojwa na Upasuaji wa Dharula, katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa, Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Nyasa Bw.Sixmund Maseti Ndunguru amesema, mara baada ya Uzinduzi huo, wamejipanga kuhakikisha kuwa, watatoa Huduma Bora kwa Wananchi wa Wilaya ya Nyasa wapatao 140,000, na wananchi wa wilaya jirani za Nchi ya Msumbiji, kupunguza Vifo vitokanavyo na Uzazi kwa kutoa Huduma Za dharula za upasuaji, kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa kutoa huduma elimu za afya na matibabu bora ya Ugonjwa wa kisukari , shinikizo la Damu, kansa kwa kuanzisha kliniki za kila wiki.

Amezitaja huduma zingine ni  Dawa muhimu na Vitenganishi vya maabara kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kununua Dawa,Vifaatiba na Vitendanishi kwa wakati.

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Nyasa wameipongeza Serikali kwa Kuwatatulia changamoto ya Huduma za kulazwa wagonjwa na Upasuaji wa Dharula kwa kuwa awali Hudumahizi walikuwa wakisafiri Umbali Mrefu wa Kilometa 150 kupata matibabu katika hospitali ya Peramiho na songea.

Halmashauri ya Nyasa imekamilisha majengo saba ya awali ya Utawala, maabara, stoo ya dawa,mionzi,wodi ya wazazi,na jingo la kufulia, njia za kuunganisha majengo,Ujenzi ambao umegharimu Tsh Bilioni 2.291, na ujenzi wa Wodi ya Wanaume wanawake na watoto Unaendelea.Mradi huu wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unatarajiwa kuwa na majengo 22 ambayo yatagharimu Tsh Bilioni 7.5.

Imeandaliwa na

 Netho C. Sichali

 Afisa Habari Nyasa Dc 0767417597.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.