• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

HALMASHAURI ya Nyasa yatoa Mikopo ya Milioni 37

Posted on: December 31st, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imetoa mkopo wa pikipiki 5, na fedha Taslim Sh Milioni 37 kwa ujumla,kwa Vikundi vya wajasiliamali vya Wanawake walemavu na Vijana .

Hafla ya kuwakabidhi wanakikundi hao imefanyika hivi karibuni,  katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, na Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas.

Akikabidhi Mikopo hiyo kwa wanakikundi, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kanali Laban Thomas ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, kwa kutoa mikopo hiyo kwa wajasiliamali ikiwa ni Fedha za asilimia kumi ya mapato ya Ndani, ambayo hukusanya Halmashuri na kuyapa makundi hayo maalum kwa lengo la kuongeza kipato kwa jamii.

Ameongeza kuwa Halmashauri imepiga hatua kubwa ya Kumkopesha Mlemavu mmoja pesa Taslim,Pikipiki 5 kwa kikundi cha Vijana na Wanawake wakipewa mkopo wa fedha Taslim.

Ametoa mchanganuo wa ugawaji wa mikopo kwa wanawake wamekopeshwa tsh 14,800,000 vijana Pikipiki 5 zenye thamani ya Tsh Milioni 13,500,000 na walemavu 8,7000,000

Aidha ametoa wito kwa wanavikundi hao kuthamini mchango wa Halmashauri, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ,hivyo wanatakiwa kurudisha fedha hizo kama mikataba yao inavyosema, ili fedha hizo zikirudishwa kwa wakati ili waweze kupewa wanakikundi wengine kwa lengo la kupanua wigo na kujilea maendeleo.

“Rai yangu kwenu ni kuhakikisha kuwa wote waliopewa fedha wanatakiwa kurudisha kama mikataba yao inavyosema, ili na wengine nao wawe wanapewa mikopo hiyo”.

Awali akitoa Taarifa fupi Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya  nyasa, Ndugu Jimson Mhagama amesema Halmashauri ya Nyasa kwa sasa imejiwekea malengo ya kutoa mikopo ya vitu,  Badala ya Fedha Taslimu ambazo haziwanufaishi walengwa kwa kuwa wanagawana kidogo kidogo na hawafikii malengo waliyojiwekea, lakini kama watapatiwa mikopo ya Vitu Kama Pikipiki, au mashine ya kusaga ili yaweze kutoa huduma na kuajiri wanakikundi wengine kama kuchakata unga na kazi zingine watafanikiwa zaidi.

Akifafanua Kuhusu utoaji Mikopo amesema tangu Halmashauri ianze haijawahi kutoa mikopo ya Vitu kama Bodaboda na Mlemavu Mmoja, kwa hiyo leo ni siku ya Kihistoria Wilayani hapa na tunashuhudia Halmashauri ikiwainua kiuchumi makundi maalum ya Vijana, Watoto, na Wanawake.

Amezitaja Kata zilizonufaika ni Liwundi, Lituhi, Mbaha,Liuli, na Kilosa.

Na kwa upande wao wanakikundi wanufaika wa mikopo hiyo wamesema wanaipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwapa mikopo hiyo na wameahidi kuitumia vizuri ili kuongeza ukuaji wa biashara zao.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.