• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

HALMASHAURI YA NYASA YAGAWA MICHE YA KAHAWA KWA WAKULIMA

Posted on: January 29th, 2020

Wakulima wa zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa kushirikiana na Vyama vya Msingi vya mazao na watu binafsi, wamezalisha miche ya kahawa 262,500 kwa msimu wa kilimo 2019/2020 ili kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa na kukuza uchumi  wa wananchi.

hayo yamesemwa na wakulima wa zao la kahawa katika Risala yao, kwa mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela O.Chilumba, wakati akizindua ugawaji wa miche mipya  ya kahawa aina ya “Compact” Uzinduzi uliofanyika  Hivi karibuni, katika Kijiji cha Kingerikiti Kata ya Kingerikiti Wilayani hapa.

Wakulima hao wamefafanua kuwa, wamelazimika kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa ikiwa ni pamoja, na utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Cassim Majaliwa aliyezitaka kili Halmashauri Nchini kuzalisha miche ya kahawa zaidi ya laki mbili.

Waliongeza kuwa Vyama saba vya Ushirika wa mazao vimezalisha miche hiyo na tayari kwa kugawa kwa wananchi kwa mchanganganuo ufuatao Nambawala AMCOS (10250), Kingerikiti AMCOS miche( 37,705), Tingi AMCOS (4,300) LIPO AMCOS MICHE (40,000), Mapendo AMCOS Miche (36,000) na Luhangarasi AMCOS 9890.

Pia wakulima hao walikipongeza kituo cha utafiti cha Ugano (TACRI) kwa kuwagawia bure miche kahawa 18,200 aina ya  compact, ambayo wameigawa kwa wakulima  ambao wanauhitaji wa miche hiyo.

Akitoa maelekezo ya upandaji wa miche hiyo kwa wakulima wa zao la kahawa, Ofisa kilimo wa Kata ya Kingerikiti ambaye pia ni Mkaguzi wa zao la Kahawa Bw.Richard Katale, aliwataka wakulima, kulihudumia vizuri, kwa kupanda kwa nafasi ya Meta mbili na kwa Hekari moja watapanda meche mia sita.

Aliongeza kuwa sifa za mche wa compact unazaa mapema na unavumilia ukame. Alikawataka wananchi  kupanda kwa maelekezo aliyoyatoa, ili kufikia uzalishaji wenye tija kwa kuwa Serikali imedhamiria kuboresha maisha ya wakulima wa zao la Kahawa.

Aidha wakulima hao, waliipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya maboresho mbalimbali ya zao la kahawa, na kuwaletea mnada wa kahawa katika Wilaya ya Mbinga na kuwapunguzia usumbufu kwa kuwa awali walikuwa wakienda moshi kufanyia mnada.

“kwa kweli awamu hii tunaona jinsi gani Serikali inatujali wakulima, kwa kuwa tunapewa mafunzo ya kulima kahawa, lakini pia kitendo cha kutupa miche ya ya kahawa bure , Serikali imetusaidia sana. Nimejaribu kupanda na nimeona ni mbegu nzuri inayotoa mavuno mengi kwa muda mfupi ukilinganisha na kahawa tuliyozoea kupanda awali”. Alisema Bonus mapunda mkulima wa zao la kahawa kutoka katika kijijii cha kingerikiti.

Akizungumza na wakulima wa zao la Kahawa Wilayani hapa, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Bw.Menance Ndomba aliyemwakilisha mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi,Isabela Chilumba,Aliwapongeza wakulima wa Zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa juhudi wanazozifanya za kulima na kutunza zao hilo na kuinua mapato ya Halmashauri na kuwa na kipato bora cha Familia na kuchangia maendeleo mbalimbali katika maeneo yao.

Aidha aliwataka kuendelea kuongeza uzalishaji wa zao la Kahawa kwa kuwa , Wilaya ya Nyasa ina Fursa ya  mashamba makubwa, kwa mujibu wa Utafiti uliofanyika hivi karibuni na “CAFE Afrika” katika Wilaya ya Mbinga na Nyasa Wilaya ya Nyasa ina fursa kubwa ya kupanua mashamba ya kahawa ukilinganisha na  Wilaya ya Mbinga.

“nachukua fursa hii kuwapongeza sana wakulima wa zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujituma kulima na kuzalisha zao hili la kahawa ambalo linatupa faida kubwa sana katika Halmashauri yetu kama vile ,mapato ya ndani na mnachangia maendeleo mbalimbali katika maeneo yenu.Serikali ipo pamoja nanyi na itatatua changamoto mbalimbali mtakazokutana nazo katika shughuli zenu na kuhakikisha Miundombinu inajengwa. Alisema ndomba.

Wilaya ya Nyasa ipo katika Mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara ya Kahawa,kakao, na korosho ili kukuza uchumi wa kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla.

Imeandaliwa na

Netho c. Sichali

Ofisa habari

Wilaya ya Nyasa 0767417597

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.