• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

ELIMU na vifaa vilivyowezesha wananchi Tunduru kuwadhibiti Tembo waharibifu

Posted on: October 11th, 2021

SHIRIKA la  kimataifa la Uhifadhi (WWF),limetoa elimu na vifaa katika vijiji vitano vilivyoathirika na tembo waharibifu wa mazao Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,ili kuwadhibiti wanyama hao.

Mhifadhi kutoka  WWF Deogratias Kilasara amevitaja vijiji vilivyonufaika na mradi huo kuwa ni Misiaji, Mpanju, Malumba,Mbati na Machemba ambapo amesisitiza WWF imedhamiria kuhakikisha tembo waharibifu wanadhibitiwa bila madhara.

‘’Wilaya ya Tunduru imekuwa na matukio mengi ya tembo waharibifu wanaovamia maeneo ya mashamba na makazi ya binadamu,WWF inashirikiana na wadau wengine kuhakikisha kuwa haya matukio yanapungua kwa kutoa elimu na vifaa vya kukabiliana na tembo’’,alisisitiza.

Amesema katika msimu uliopita WWF ilitoa elimu ya matumizi ya pilipili na uzio wa kitambaa kwa kutumia mafuta machafu na kutoa matokeo mazuri ambapo amekitaja kijiji cha Misiaji kuwa cha mfano wa kuweka uzio kuzui tembo katika mashamba.

Hata hivyo amesema WWF imetoa mabomu 400 ya kufukuza tembo waharibifu wilayani Tunduru kwa ajili ya matumizi msimu ujao wa kilimo.

Wakizungumza namna walivyonufaika na elimu ya kukabiliana na tembo waharibifu wa mazao katika msimu uliopita,wananchi wa kijiji cha Misiaji Tunduru wamelishukuru Shirika la WWF kwa elimu hiyo ambayo imewawezesha kuvuna mazao yao bila kuathiriwa na tembo.

Said Amigo Mkazi wa Misiaji Tunduru amesema  baada ya kupata elimu,aliweka  uzio wa pilipili kwenye shamba lake la mahindi na viazi ambapo amefanikiwa kuvuna mahindi gunia 36 na viazi  anaendelea kula hadi sasa na kwamba tembo wanafika lakini hawaingii kwenye mashamba yake.

Rashid Kassim Mkazi wa Misiaji na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chingoli Tunduru amesema katika msimu uliopita walifanikiwa kufunga uzio wa pilipili kwenye mashamba ya vijiji vya Misiaji  na Malumba kupitia ufadhili wa WWF na kwamba tembo walipofika kwenye mashamba yenye uzio hakuna shamba lililoshambuliwa.

Amesema wakulima kutoka vijiji hivyo wameamini na kuridhika kuwa pilipili na mafuta machafu ni kiboko ya tembo waharibifu wa mazao kwa sababu mazao yao yamesalimika.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Agustino Maneno  amewapongeza WWF kwa mafunzo ya kukabiliana na tembo waharibifu ambayo yamewawezesha wananchi kuvuna mazao yao katika msimu uliopita.

“Nawapongeza sana kwa msaada wa mafunzo na mabomu 400 ya kufukuza tembo waharibifu,hata hivyo kwa ukubwa wa wilaya na changamoto iliyopo kwa mwaka walau tunahitaji mabomu 200 kukabiliana na tembo waharibifu’’,alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Mheshimiwa Daim Idd Mpakate  amewashukuru WWF kwa kutoa elimu na vifaa vya kukabiliana na tembo waharibifu ambapo amesema idadi ya tembo watapungua na kwenda kwenye maeneo yao ya asili .

Mbunge wa Tunduru Kaskazini Mheshimiwa Hassan Myao ametoa rai kwa WWF kushirikiana na TAWA TANAPA,TFS na wadau wengine wa mazingira kutafuta njia nyingine mbadala za kukabilina na tembo waharibifu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 8,2021

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.