• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

DED NYASA AWATAKA WALIMU KUFUNDISHA KWA BIDII NA KUEPUKA UDANGANYIFU MITIHANI.

Posted on: February 23rd, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma leo,  imefanya Kikao kazi  cha Siku moja Kwa Walimu wakuu, walimu wa Taaluma na Maafisa Elimu kata, kikao chenye lengo la kuwajengea Uwezo washiriki hao kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mafunzo yamefanyika katika Ukumbi wa Kassim majaliwa uliopo katika Shule ya Sekondari Mbamba bay, ilyopo katika Kijiji cha Ndengere Kata ya Mbamba bay Wilayani Hapa.

Akifungua Kikao kazi, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama amewataka Washiriki kuwaandaa wanafunzi kwa kuwafundisha mada zote, zinazotakiwa kufundishwa ili kuwaandaa vema na mitihani ya kiwilaya na kitaifa ili kujiepusha na Udanganyifu katika kipindi cha Mitihani.

Ameongeza kuwa kuwaandaa wanafunzi vizuri, kwa kuwafundisha mada zote, anazotakiwa kufundisha kwa mwaka mzima, na mazoezi ya mara kwa mara ni njia pekee ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu, kwa kiwango cha juu na kuandaa wataalam wazuri watakaojenga Taifa la Tanzania kwa miaka ijayo, waliondaliwa vizuri na kufaulu mitihani.

Aidha amesema Halmashauri itawachukulia hatua za kinidhamu na Kisheria mwalimu yeyote atakayesababisha, aidha kushusha taaluma Wilayani hapa au kusababisha udanganyifu wa Mitihani yote ya Ndani ya Wilaya,  Mkoa na kitaifa.

“ndugu Walimu nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya, na kuhakikisha Wilaya ya Nyasa inafaulisha wanafunzi. Nachukua Fursa hii kuwataka kutekeleza majukumu yenu vizuri, kwa kuwafundisha wanafunzi mada zote unazotakiwa kufundisha na kujiepusha na Udanganyifu wa Mitihani, kwa kuwa umewaandaa vizuri wanafunzi wako. Mimi kama mwajiri wenu nimewaita ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yenu, katika Shule zenu kwa kuwa kazi ya mwalimu ni kufundisha na wanafunzi wafaulu Mitihani. Aidha sitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa walimu ambao hawatatekeleza kwa majukumu yao”

Awali Ofisa Elimu Msingi wilaya ya Nyasa Bw. Said Kalima, akitoa Takwimu za Ufaulu Wilaya ya Nyasa kwa Miaka Miwili Mfululizo, amesema  wilaya imepanda, kwa ufaulu kwa darasa la nne, kwa mwaka 2019 wilaya ilipata wastani wa asilimia 96.2,  na mwaka 2020 tulikuwa na wastani wa 96.4, na darasa  la saba wilaya kwa mwaka 2019 ilikuwa na wastani wa asilimia 78.81 na kwa mwaka 2020 wilaya imepata wastani wa asilimia 83.2 na kusema haya ni mafanikio makubwa sana yaliyofanywa na walimu wa Nyasa na kuwapongeza kwa uchapakazi wao.

Aidha amewataka Walimu hao kuongeza juhudi za kufundisha kwa kumaliza mada ili kuendelea kupandisha ufaulu na kufikia asilimia 100, kwa mwaka 2021,   kwa kuwa matokeo ya mwaka jana yameshapita hivyo kwa sasa ni maandalizi ya kuongeza ufaulu kwa mwaka huu, hivyo kuna kila sababu ya kukumbushana.

Bw Kalima amesema kuwa ili kuboresha Utendaji kazi wa Viongozi kwaka 2021, Idara ya Elimu Msingi  imewaandalia mkataba maalum  kati ya Viongozi hao wa kata na Shule ili kuwapima kwa malengo waliyopewa, na jinsi alivyotekeleza. Aidha kwa ambaye hatatekeleza mkataba huo atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo waesema Kikao kazi hicho kimewakumbusha majukumu yao, na watayatekeleza ili kuifanya Wilaya ya Nyasa iwe juu kwa kuwaandaa wahitimu wenye Taaluma bora na kuleta Tija katika Taifa la Tanzani.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.