• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

DC Nyasa awataka wafanyabiashara Nyasa kushikamana na kuzitumia fursa ipasavyo

Posted on: August 17th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas Leo, amewataka wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa kushikamana, kupendana na kuzitumia fursa za kibiashara zilizopo Wilayani Nyasa katika kujipatia maendeleo.

Ameyasema hayo  wakati akiongea na Wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa katika Kikao chenye lengo la kujitambulisha na kuzitambua kero zinazowakabilki wafanyabiashara Wilayani hapa.

Kanali Thomas amefafanua kuwa, Wilaya ya Nyasa hususani katika Mji wa Mbamba bay ni miongoni mwa miji iliyofunguka na inayokua kwa kasi, hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kushikamana ,kupendana, na kuzitumia fursa za kibiashara ili kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutanua Mji na kuacha kufanya biashara sehemu moja, kimazoea yaani Mbamba bay peke yake na badala yake watanue mji.

Ameongeza kuwa Mji wa Mbamba bay ni pamoja na Kata ya Kilosa na Mtipwili na kwa sasa Makao makuu ya Mji wa Mbamba Bay ni Kilosa, Hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kuanzisha biashara mbalimbali mpya katika Kata ya Kilosa na kuacha kubanana katika Mji mkongwe wa Mbamba bay ili watanue Fursa za kibiashara.

“wafanyabiashara kwa mnatakiwa mpendane,mshikamane ili muweze kuzitumia Fursa za kibiashara zinazokuwa kwa kasi katika Mji wa mbamba bay Wilayani Nyasa, acheni tabia ya Ubinafsi ili muweze kupata maendeleo kwa kasi, katika Mji ambao unakuwa kwa kasi mara baada ya kufunguka kwa barabara ya Mbinga hadi Mbamba bay, na kufungua fursa za Biashara mbalimbali.

Wafanyabiashara hao wametaja baadhi ya Changamoto zinazowakabili ni pamoja na bandari ya mbamba bay kutofanya kazi ya kupitisha mizigo, kutoka Mtwara hivyo wafanyabiashara hao wamemuomba mkuu wa Wilaya kutoa msukumo kwa Serikali ili iharakishe,  kuzifanya meli zifanye safari na Mizigo ya kutoka Mtwara kuja Mbamba bay ianze  kuja, ili wafanyabiashara waweze kunufaika na kufanya  biashara.

Kero Nyingine inyowakabili wafanyabiashara hao ni makadirio ya kodi yanayofanyika na Mamlaka ya mapato Tanzania kukadiriwa wakiwa Ofisini badala yake wameomba maafisa wa kodi waende katika eneo la biashara ili waweze kukadiriwa vizuri.

Aidha Mkuu wa Wilaya ametatua kero hizo kwa kuwaagiza maafisa wa kodi kufanya makadirio katika maeneo ya Biashara, na kuwaeleza kuwa suala la Bandari atalifikisha katika Mamlaka husika.

Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kufanya biashara halali na kuhakikisha ulinzi na usalama aidha wanapomtilia mashaka mtu yeyote basi weatoe taarifa mapema katika vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.