• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

Posted on: April 30th, 2025

MADIWANI NYASA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATUMISHI KUIBUA VYANZO VIPYA VYA MAPATO

MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Peres Magiri,amewataka Madiwani kushirikiana na Watumishi wakiwemo watendaji wa Vijiji na Kata waliopo  kwenye maeneo yao kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vilivyopo  ili kuijengea uwezo Halmashauri  yao kujitegemea na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Magiri ameyasema hayo hivi Karibuni wakati akitoa salamu za Serikali kwenye kikao cha robo ya tatu cha Baraza Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambacho kimehudhuriwa na watendaji kata,wakuu wa idara na Madiwani.

“Halmashauri ikiwa na vyanzo vingi zaidi vya mapato itakusanya fedha nyingi na  kutoa huduma bora za kijamii kwa Wananchi ikiwemo huduma za afya,elimu na kuongeza mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu”alisema Magiri.

Aidha,ametaka ukusanyaji wa mapato lazima uendane na nidhamu ya matumizi ya fedha na Madiwani  kuhakikisha wanasimamia mapato yanayopatikana kupitia vyanzo mbalimbali yanatumika ipasavyo.

“Madiwani kupitia kamati zenu muwe na utaratibu wa kufuatilia na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili kujiridhisha kama inalingana na fedha zinazotolewa na Serikali badala ya kuwa watazamaji”alisema Magiri.

Magiri,amewataka watumishi wapya kwenda kufanya kazi kwa kujituma ili kuleta imani kwa Wananchi ambao wana mategemeo  makubwa kupata huduma bora  kutoka kwao na kujiepusha na tabia zinazokwenda kiunyume na maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kuzalisha migogoro na chuki kati ya Serikali na Wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa Khalid Khalif alisema,kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wamepangiwa kukusanya Sh.bilioni 2.4 sawa na ongezeko la asilimia 66 kutoka bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Khalif alisema,hadi kufikia tarehe 30 Machi  wamekusanya Sh.bilioni 1.8 sawa na asilimia 78.36  na hadi kufikia tarehe 28 Aprili 2025  wamekusanya zaidi ya asilimia 82 ya mapato yake ya ndani yaliyokusudiwa kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Alisema,kwa mwaka ujao wa fedha 2025/2026 utakaoanza tarehe 30 Juni Halmashauri hiyo imepangiwa kukusanya jumla ya Sh.bilioni 3.2 ikiwa ni ongezeko la asilimia 35 kutoka bajeti  inayoendelea kutekelezwa kwa sasa.

Kwa mujibu wa Khalif,ili kufikia malengo waliyojiwekea Halmashauri imeweka mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato na kudhibiti upotevu ikiwemo uchimbaji wa makaa ya mawe kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji watakaokwenda kuchimba makaa  hayo katika Wilaya ya Nyasa.

Alitaja mikakati mingine ni pamoja na Halmashauri kununua leseni 20 kwa ajili ya kuanza kuchimba makaa ya mawe na wametenga Sh.milioni 20 kwa ajili ya kufanya biashara ya makaa ya mawe yanayopatikana kwa wingi katika Wilayani humo.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Stella Manyanya alisema,katika kipindi cha miaka mitano 2020-2025 watumishi wa Halmashauri wamekuwa kitu kimoja na kufanya kazi kwa  ushirikiano hali iliyosaidia  kuvuka malengo ya kukusanya mapato ya ndani na kupata hati safi.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Zefania Manyeshi,ameipongeza Halmashauri  ya Wilaya Nyasa  kwa kupata hati safi kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG)katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa Stuwart Nombo,amewasitiza Madiwani kwenda kueleza mambo mazuri waliyofanya na yaliyotekelezwa na Serikali katika kipindi cha miaka mitano ili waweze kueleweka kwa Wananchi.

 ----- Forwarded Message -----
 From: Amri Mmanja <amrimmanja@yahoo.com>To: "mharirihabarileo@gmail.com" <mharirihabarileo@gmail.com>Cc: "mauahmed@yahoo.com" <mauahmed@yahoo.com>; "bmsongo@gmail.com" <bmsongo@gmail.com>Sent: Thursday, May 1, 2025 at 07:22:51 AM GMT+3Subject: MADIWANI NYASA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATUMISHI KUIBUA VYANZO VIPYA VYA MAPATO

 Na Muhidin Amri,
Nyasa

MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Peres Magiri,amewataka Madiwani kushirikiana na Watumishi wakiwemo watendaji wa Vijiji na Kata waliopo  kwenye maeneo yao kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vilivyopo  ili kuijengea uwezo Halmashauri  yao kujitegemea na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Magiri ameyasema hayo jana, wakati akitoa salamu za Serikali kwenye kikao cha robo ya tatu cha Baraza Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambacho kimehudhuriwa na watendaji kata,wakuu wa idara na Madiwani.

MWISHO.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.