• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

DC NYASA APIGA MARUFUKU KUINGIZA BIDHAA TOKA NJE YA NCHI KWA NJIA ZA PANYA

Posted on: January 25th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela O. chilumba, amewataka Wajasiliamali na wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa kufanya biashara halali, na kulipa kodi halali, pia kuacha kuingiza bidhaa kutoka nje ya Nchi na kukwepa kulipa kodi.

Ameyasema hayo hivi karibuni, wakati akiongea na wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa katika kikao cha kujadili mambo masuala ya Biashara na maendeleo, kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Baylive uliopo Mbamba bay Wilayani hapa.

Chilumba amefafanua kuwa, wafanyabiashara na wajasiliamali wa Wilaya ya Nyasa wanakabiliwa na changamoto ya ukwepaji ulipaji kodi, na kuingiza bidhaa mbalimbali, kutoka Nje ya nchi hususani,  Msumbiji na Malawi kwa njia za panya ili kukwepa kulipa kodi halali ya Serikali, na kuikosesha nchi yetu Mapato ambayo yangeweza kujenga miundombinu ya Nchi.

Aliongeza kuwa amelazimika kuitisha kikao hicho, ili aweze kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao, ili waweze kupata elimu ya ulipaji kodi, na kutoa agizo la kuacha mara moja tabia ya kuingiza kiholela kwa njia za magendo bidhaa mbalimbali kama vile mafuta ya kupikia, yanayotoka Nchini Msumbiji na Sukari inayotoka Nchi ya Malawi.

Aidha amewataka wajasiriamali  kufuata kanuni, taratibu na sheria za kuingiza bidhaa hizo kutoka nje ya Nchi kwa kukata leseni.

“Tunachangamoto kubwa ya Wafanyabiashara wengi ya kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka Nchi ya Msumbiji na Malawi, hasa Sukari na Mafuta ya kupikia, ambayo huingia kwa njia isiyokuwa halali na kukwepa kulipa Kodi. Nichukue fursa hii kuwaambia kuwa majina ya wafanyabiashara hayo tunayo na tumekuwa tukikamata na kutaifisha pamoja na wahusika kuwachukulia hatua kali za kisheria, lakini bado wanaendelea kufanya biashara haramu. kama Serikali tuna wajibu wa kutoa elimu kwa Wafanyabiashara, ili wafuate Taratibu kama tulivyoamua kuwaita kwa siku ya leo. Ili Nchi ipate mapato ni Lazima Kila mfanyabiashara walipe kodi halali, na tutahakikisha tunawachulia hatua za kisheria, wale wote watakaokwepa kulipa Kodi ya Serikali.Alisema Chilumba.

Aidha katika hatua nyingine amewapongeza wafanyabiashara hao kwa kuchangamkia fursa za Kibiashara wilayani Nyasa kwa kuleta Bidhaa Mbalimbali na kuhakikisha kila aina ya bidhaa inapatikana katika Wilaya ya Nyasa hususani katika Mji wa Mbamba bay Ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Nyasa.

Kwa upande wao wafanyabiashara Wilayani hapa, wameiomba Serikali ya Tanzania, kupunguza ushuru na Tozo hasa katika Bidhaa za Nje kwa kuwa kinachosababisha wakwepe kulipa kodi ni kiwango kikubwa cha tozo wanachotozwa na Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA)  hali inayowapelekea wafanyabiashara hao kutopata faida.

Wameongeza kuwa kama Serikali itaweka viwango rafiki vya ulipaji kodi ya Bidhaa zinazoingia toka Nchi jirani itasaidia kufuata sheria kanuni na Taratibu za ulipaji kodi.

 Kwa upande wake Afisa Biashara wa Wilaya ya Nyasa Zaitun Hamza, amewataka wafanyabiashara hao kufahamu kuwa viwango vya  kodi wanazotozwa, ni kwa mujibu wa Sheria ya Kodi hivyo hakuna anayeweza kupunguza viwango hivyo vya kodi. Aidha amewahamasisha wafanyabiashara hao kununua na kuuza bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi ili kukuza uchumi wa Nchi yetu

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.