• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Dc Nyasa aipongeza Tarafa ya Mpepo kwa kutoa chakula Cha mchana shule zote.

Posted on: August 29th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mheshimiwa Peres Magiri ameipongeza Tarafa ya Mpepo wilayani humo kwa kufanikiwa kutoa chakula cha mchana kwa shule zake zote.

Ametoa pongezi hizo wakati anazungumza kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa  lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024 ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilosa Mbambabay.


Amewaagiza watendaji wote wa Kata na wadau wa afya na lishe kusimamia utekelezaji wa shule zote kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi ili kupunguza udumavu unaoikabili  Wilaya ya Nyasa na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.


“Nawaagiza watendaji Kata wote katika wilaya ya Nyasa,kuhakikisha shule zote zinatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi kwa sababu haya ni maamuzi yaliyopitishwa kwenye vikao vya vijiji na Kata’’,alisisitiza.


Sanjari na agizo hilo,Mkuu wa Wilaya pia ameagiza kila shule angalau iwe na bustani ya mboga ili kupata lishe bora kwa sababu,shule zinazotoa chakula cha mchana kwa wanafunzi sehemu kubwa , wanafunzi wanakula kande za mahindi yaliyokobolewa hivyo kukosa virutubisho muhimu na kusababisha udumavu kuendelea.


Taarifa ya tathmini ya Mkataba wa lishe katika Halmashauri ya Nyasa iliyotolewa katika kikao hicho,inaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024 jumla ya wanafunzi 49,161 kati ya 58,191 wanapata angalau mlo mmoja wawapo shuleni  sawa na asilimia 84.48 .


Kulingana na taarifa hiyo katika kampeni iliyofanyika Mwezi Juni mwaka huu, Watoto 23,504 kati ya 23,504  sawa na asilimia  100 walipatiwa matone ya vitamini A.


Hata hivyo taarifa hiyo inaonesha kuwa katika kipindi hicho Watoto 15 kati ya 14,665 sawa na asilimia 0,001 waligundulika na utapiamlo mkali na kwamba wote walipatiwa matibabu.


Ili kukabiliana na utapiamlo na udumavu wilayani Nyasa,baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa kwenye kikao hicho ni Pamoja na shule zote za msingi na sekondari kulima bustani za mboga,matunda na kuendelea kuhamasisha wanafunzi shuleni kutumia unga ulioongezwa virutubisho.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.