• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

BRIGEDIA JENERALI IBUGE AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA MSUMBIJI

Posted on: June 1st, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefanya ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa kwa kukagua eneo la Mkenda lililopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kupitia wilaya ya Songea.

Brigedia Jenerali Ibuge amekagua daraja la Mkenda Mto Ruvuma linalotenganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji, amezungumza na askari wa Msumbiji waliopo mpakani,ametembelea kivuko cha Mitomoni,kupitia Mto Ruvuma,amekagua soko la kimataifa la Mkenda na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mkenda.

Akizungumza na watumishi wa Idara za uhamiaji,Mamlaka ya Mapato Tanzania,polisi na Usalama waliopo eneo la Mkenda,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amelitaja lengo la serikali kuwaweka watumishi hao mpakani ni kusimamia maslahi ya taifa.

 Amewataka watumishi hao kila mmoja katika Idara yake kushirikiana na kufanya kazi kwa tija na ufanisi kwa maslahi ya watanzania.

“Sasa hili la ushirikiano nataka kusisitiza,mpo mbele ya mpaka wetu ,kumbukeni kuna changamoto kubwa ya ugaidi inayotukabili kwenye mpaka wetu na Msumbiji ,huu sio wakati wa kuchukulia vitu poa’’,alisisitiza Brigedia Jenerali Ibuge.

Hata hivyo amewatahadharisha watumishi hao wasipokuwa na muunganiko wanapobaini watuhumiwa wakiwemo wahamiaji haramu, biashara zinazotia mashaka na vitendo vya rushwa wanaweza kuharibu mfumo mzima wa Mkoa na Taifa kwa ujumla kutokana na uzembe.

Kuhusu watumishi wa TRA waliopo mpakani,RC Ibuge amesema licha ya ukweli kuwa mapato ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,hata hivyo ametaka ushirikiano wa kuangalia mazingira ya kiforodha yaangaliwe kiulinzi na usalama kwa kudumisha mawasiliano na vyombo vingine vya usalama.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa pole na kuwafariji wananchi wa kijiji cha Mkenda kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali ya majini kwenye mto Ruvuma hivi karibuni. 

Hata hivyo ametoa rai kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mkenda na wananchi kwa ujumla kushirikiana na vyombo vya usalama vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ili  kujilinda kwa ajili ya usalama wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Kituo cha Uhamiaji Mkenda,Mratibu Msaidizi wa Uhamiaji Upendo Kikudo amesema kituo hicho kinafanya kazi kwa ushirkiano na Idara nne ambazo ni  Uhamiaji,Polisi,TRA na Usalama wa Taifa.

Amezitaja changamoto zinazokikabili kituo hicho ni ukubwa wa mpaka kutokana na jiografia ya eneo lililozungukwa na Mto Ruvuma na misitu,hali ya machafuko inayoendelea nchini Msumbiji,uwepo wa vipenyo vingi vilivyo rasmi na visivyo rasmi,mawasiliano,miundombinu ya barabara,huduma za afya na ukosefu wa nishati ya umeme.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.