• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

BARAZA LA MADIWANI NYASA LAPITISHA BAJETI YA TSH BILIONI 22.7

Posted on: March 5th, 2021

Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, leo  limepitisha Bajeti ya  yenye thamani ya shilingi bilioni 22,709,154,050.00,  kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri, katika  kikao kilichofanyika , Ukumbi wa Kepten John Komba Uliopo Mbamba bay Wilayani hapa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Stewart Nombo,  ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Madiwani amesema kuwa baraza  limeidhinisha mpango na bajeti ya maendeleo, kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kwa kuwa bajeti hii imelenga kutatua kero mbalimbali za wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza Miradi ya Maendeleo, na kutoa wito kwa  madiwani  kutoa ushirikiano kwa wataalamu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata zao.

Akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022,  Kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Nyasa, Ofisa Mipango wilayani wa Wilaya Bw. Jabir Chilumba amefafanua kuwa bajeti hiyo, inalenga kutekeleza Program mbalimbali zilizopangwa kufanyika katika Halmashauri. Kati ya Kiasi hiki Tsh 1,237,512,500.00 sawa na Asilimia 5.45, ni makusanyo ya ndani, Tsh 13,283,311,000.00 sawa na Asilimia 58.49 ni kwa ajili ya Mishahara, Tsh 1,425,032,000.00 sawa na asilimia 6.28 kwa ajili ya matumizi mengineyo, na  Tsh 6,763,298,550.00 sawa na asilimia 29.78 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama,  amewataka madiwani wa Wilaya ya Nyasa kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kushirikiana na wananchi, kutekeleza miradi hiyo na kusema kuwa Miradi hii inatekelezwa kwa fedha za walipa kodi, kwa hiyo ni jukumu la kila kiongozi kusimamia fedha hizo ili kujiletea maendeleo.

“waheshimiwa  madiwani ninawataarifu kuwa kila ninapokuandikia na kukupa taarifa za kukuletea fedha katika eneo lako, ni jukumu lako kusimamia, kuwashirikisha wananchi, na kutekeleza miradi kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuwa fedha zinazotekeleza miradi hii ni kodi za wananchi wetu na Mh Rais amezileta ili zitatue changamoto za wananchi hivyo kila kiongozi anatakiwa kuwajibika kwa nafasi yake” .

Mhagama amesisitiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, inatekeleza mpango mkakati wa kuongeza mazao ya kilimo na Biashara kwa kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa, michikichi, Cocoa, Korosho na mazao mengine ili wananchi wanufaike na mazao ya kimkakati na Halmashauri iweze kupata mapato yanayotokana na mazao hayo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya,  amesema Wilaya ya Nyasa ina mazao bora yasiyotumia mbolea za kiwandani, hivyo mazao hayo kwa sasa yamepata umaarufu mkubwa hasa  kwa   zao la kahawa, wanywaji wengi wa kahawa hawahitaji kahawa iliyolimwa kwa mbolea za kiwandani, wanahitaji mazao yaliyolimwa kwa kutumia samadi hivyo kwa Wilaya ya Nyasa tunatakiwa kutumia Fursa hiyo kwa kuvutia wawekezaji ili tuweze kujipatia maendeleo.

Aidha  amepongeza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama, na Wataalamu wake, walioshiriki kuandaa mpango na bajeti  ambayo imezingatia vigezo  muhimu vyenye lengo la kutatua Kero za wananchi Wilayani Hapa.


Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.