• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

ASLIMIA 90 YA VITABU VYA TANZANIA HAVINA MAUDHUI YA UKWELI KUHUSU UHURU WA TANZANIA

Posted on: August 17th, 2020

Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo,  Dkt Harrison Mwakyembe amesema asilimia 90 ya vitabu vya Tanzania havina maudhui ya ukweli kuhusu Tanzania ilivyopata uhuru wake bila kumwaga damu .

Waziri Mwakwembe ameyasema hayo wakati alipotembelea Makumbusho ya Taifa ya  Majimaji Mjini songea hivi karibuni katika ziara yake aliyoifanya mkoani Ruvuma ya kutembelea maeneo ya  harakati za ukombozi dhidi ya wakoloni.

Amesema suala la kupata uhuru ni mchakato ,hivyo uhuru wa Tanzania haujapatikana kwa njia ambazo waandishi wa vitabu  wamezitaja  kwa sababu kuna wananchi walijitolea katika harakati za ukombozi hadi kumwaga damu.

Dkt.Mwakyembe akiwa katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji alishuhudia historia ya ukombozi iliyoanza wakati wa Vita vya Majimaji iliyofanyika mwaka 1905 hadi 1907  ambapo katika vita hivyo mashujaa 67 walivyongwa na kuzikwa kwenye makaburi yaliyopo ndani ya makumbusho hayo..

Kulingana na Mwakyembe,vitabu vingi vya Historia ya Upatikanaji wa Uhuru ya Tanzania inaonesha kuwa Tanzania bara ilipata Uhuru bila kumwaga damu jambo ambalo amesema sio sahihi kwa sababu tangu miaka ya Vita vya Majimaji Wananchi wa Tanganyika waliukataa Utawala wa Wajerumani ambao walikuwa wanaitawala Tanzania wakati ule ambapo baadhi yao walipoteza maisha kwa kumwaga damu.

“Mababu zetu walipigania uhuru kwa kumwaga damu kwa lengo la kupinga Utawala wa Wajerumani na ndipo walipoanzisha vita ya Majimaji na kupigana tangu mwaka 1905 hadi 1907 na ndipo mashujaa wa vita vya majimaji 67 walinyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja’’,alisisitiza.

Hata hivyo amesema vitabu vingi historia havionyeshi Tanzania ilipata Uhuru kwa Kumwaga damu,badala yake vitabu vinaonesha Tanzania ilipata Uhuru bila kumwaga Damu jambo ambalo Waziri Mwakyembe amesema  hakubaliani na waandishi wa Historia ya Tanzania.

“Kwa kweli hapo sikubaliani na waandishi wa Historia ya Tanzania nafikiri waanzie mwanzo kabisa badala ya kuanzia  wakati wa Uhuru’’,alisisitiza Dkt.Mwakyembe.

Dkt.Mwakyembe ameagiza kutunzwa kwa makaburi ya Mashujaa  67 waliozikwa katika Kaburi moja ndani ya Makumbusho ya Majimaji na kwamba mashujaa hayo walipinga Utawala wa Wajerumani.

Amesema wakoloni walikuwa wanyonyaji ambao  waliwatumikisha wananchi kwa ujira mdogo na kulipa kodi  kwa manufaa ya Utawala wa Ujerumani.

 Waziri Mwakyembe ameshauri  waandishi wa vitabu vya historia waanzie toka enzi za vita ya Majimaji vilivyopigana katika Mikoa nane ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Ruvuma na kuonesha idadi ya mashujaa waliomwaga damu.

Pia Mwakyembe ameshauri Wanafunzi kwenda kujifunza uhalisia wa vitendo,picha mbalimbali na vifaa halisi vilivyotumika katika vita ya Majimaji kwenye Makumbusho ya Taifa ya Majimaji.

Imeandikwa na Netho Credo na Jackline Clavery

Maafisa Habari Serikalini

Agosti 17,2020

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.