• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

AKINA MAMA WAPATA HAMU YA KUZAA NYASA

Posted on: May 13th, 2020

Akina mama  wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma wamesema wamepata hamu ya kuzaa, baada ya kukabidhiwa rasmi Gari ya kubebea wagonjwa ya Kituo cha afya Mbamba-bay.

Gari hiyo imekabidhiwa jana katika Kituo cha afya cha Mbamba-bay Wilayani hapa na Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stela Manyanya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na kupokelewa na Uongozi wa Kituo cha afya Mbamba-bay Wilayani hapa.

Akinamama hao walimueleza mbunge kuwa ,Hamu ya kuzaa imeongezeka kutokana na kupewa gari mpya ya kubebea wagonjwa, kwa kuwa mwanzo walikuwa wakikumbana na adha ya Uzazi pale wanaposhindwa kujifungua na kulazimika kupata gharama nzito ya kukodi gari ili kwenda, Hospitali kubwa kwa uchunguzi zaidi.lakini kwa sasa, hawana tena wasiwasi kwa kuwa gari ipo.

“Tunaishukuru sana Serikali ya Rais John pombe magufuli, na mbunge wetu wa Nyasa  kwa kutuletea gari ya Wagonjwa   katika kituo chetu cha afya cha Mbamba-bay, Awali tulikuwa hatuna hamu ya kuzaa kwa kuwa tulikuwa tukuhofia usalama wetu wa afya ya uzazi kama tulikuwa tukipata matatizo ya Uzazi kulikuwa hakuna usafiri wa uhakika wa kutufikisha hospitali kubwa lakini kwa sasa Hamu ya kuzaa imeongezeka kutokana na kukabidhiwa gari jipya ambalo tumekabidhiwa leo”.alisema mariana Kapinga

Awali akitoa Taarifa fupi  ya Kituo cha Afya kwa Mgeni Rasmi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbamba-bay Michael Mabisi alisema Kituo hicho kwa sasa kinaendelea vizuri na changamoto nyingi za vifaa tiba na vitendea kazi viko katika Hali nzuri na kumpongeza Mh. Mbunge kwa mchango mkubwa wa kukiboresha Kituo cha Afya cha Mbamba-bay na Wilaya ya Nyasa kwa ujumla wake.

“Mh Mbunge sisi wafanyakazi wa kituo cha Afya Mbamba-bay tunatambua mchango wako wa hali na mali wa kuboresha sekta ya Afya, Hususani kuboresha Kituo hiki kwa kutatua changamoto nyingi zilizokuwa inakikabili na Leo hii umetukabidhi gari la Wagojwa tunakushukuru sana.Kama wafanyakazi tunatembea kifua mbele kwa kwa tuna Mbunge anayejali Watumishi, anayejali afya ya Jamii”Alisema Dkt  Mabisi.

Akikabidhi Gari ya Wagojwa Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stela Manyanya,  Alisema anamshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe magufuli kwa kuwajali wananchi wa Nyasa , kwa kutupa miradi mbalimbali ya Afya kwa kuwa tumejengewa Hospitali ya Wilaya na Vituo vya afya vya Mkili, Kihagara, Kingerikiti na Kuboresha Miundombinu ya Vifaa tiba ,na Miradi mingine mingi ya Maendeleo kwa Wilaya ya Nyasa.Inaonyesha ni jinsi gani anatupenda Wananyasa na leo hii ametupatia gari ya Wagonjwa mpya ambayo itasaidia kubeba wagonjwa na shughuli zingine za Afya.

Amewataka Uongozi wa Afya kituoni hapo kulitunza gari hilo ili liweze kuwa zima muda wote kwa kuwa gari ni mali ya Wananchi na Dereva atakayepata alitunze atembeze kwa uangalifu na kutunza Siri za akina mama hao.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.