• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

AFISA MWANDIKISHAJI WA JIMBO NYASA AWATAKA MAAFISA WAANDIKISHAJI NGAZI YA KATA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Posted on: January 5th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa tarehe 05/ na 06/01/2025 inatoa Mafunzo ya Siku mbili kwa Maafisa Waandikishaji Ngazi ya Kata, yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Nyasa.

 Lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa Waandikishaji Ngazi ya Kata, kwa ajili ya kuboresha Daftari la kudumu la Wapiga Kura Wilayani Nyasa. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 12 – 18 Januari, 2025.

Akifungua mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Nyasa Bw. Khalid A. Khalif amewataka washiriki wa mafunzo kusikiliza mafunzo kwa makini kwa kuwa yanawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Amefafanua kuwa, Mafunzo haya yatahusisha namna ya ujazaji fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura, (Voters Registration System- VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha Wapiga Kura hivyo basi mnatakiwa kuwa makini na kuelewa mafunzo.

“Mafunzo haya yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Waandikishaji Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki ambao ndio watahusika na uandikishaji wa Wapiga Kura Vituoni”.

Aidha, amewaagiza Maafisa hao kuwa wakati wa Uboreshaji wa Daftari mawakala wa Vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura. Hivyo, basi mnatakiwa kuzingatia ili kuleta uwazi katika zoezi zima na kuwatambua waombaji katika maeneo yao, ila mawakala hao wasiingilie majukumu ya Watendaji.

Amewataka kutunza vifaa, kushirikiana na maafisa Ngazi ya Jimbo na kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo wakiongozwa na Mwenyekiti wao wamesema watasikiliza mafunzo hayo kwa umakini  na kufanya kazi kwa weredi.

Awali kabla ya kuanza mafunzo Mhe.Zuberi Kigwangala, Hakimu Mkazi wa mahakama ya Mwanzo Mbamba bay amewaongoza washiriki kula kiapo cha kutunza siri na kutoa Tamko la kujitoa Uanachama au kutokuwa na Mwanachama wa Chama cha Siasa

Imeandaliwa na

Netho Credo Sichali

AFISA HABARI WILAYA YA NYASA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • Wilaya ya Nyasa yaadhimisha miaka 61 ya Muungano kwa Kufanya Usafi

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.