• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

AFISA ARDHI NYASA AMWOKOA MJANE ALIYEFUKUZWA NA WATOTO WAKE, ILI WARITHI MALI ZA MAREHEMU BABA YAO.

Posted on: May 20th, 2021

Mali iliyochumwa na wanandoa wawili (matrimonial property) mmoja akifa umiliki unahamia kwa mwanandoa aliyebaki, na watoto hawana haki ya kugawana wala kudai chochote kwa kuwa sheria haiwatambui watoto isipokua kama wazazi wameamua kuwagawia watoto.

Hayo yamesemwa na Afisa Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ambaye Kitaaluma  ni mwanasheria Bw. Philoteus J. komba wakati akisuluhisha mgogoro wa Mjane Mariam Gama aliyefukuzwa na mwanae Feruzi Miteo ili arithi ardhi ya marehemu baba yake, hivi karibuni  katika Ofisi ya  Kijiji cha Mango Kata ya Kihagara Wilayani Nyasa.

Afisa ardhi huyo amefafanua kuwa, sheria haiwatambui watoto katika mali za wanandoa hivyo mwanandoa mmoja akifariki umiliki wa mali unahamia kwa mwanandoa aliyebaki na hatakiwi kubugudhiwa, kwa kuwa sheria inamtambua kuwa ni mmiliki halali na watoto watakuwa na uhalali ikiwa wazazi wote wawili wamefariki.

Aidha amemtaka Kijana huyo Ferudhi Miteo  kuacha mara moja kumnyanyasa  na kumfukuza mama yake katika maeneo yake kwa kuwa ni mmiliki halali na Sheria inamtambua. Amewaelekeza Viongozi wa Vijiji kumchukulia hatua za kisheria mara moja endapo akiendelea na tabia ya kumnyanyasa mjane huyo.

Awali mjane Mariam Gama (70) aliwasilisha malalamiko kwa Kamishina wa Ardhi Msaidizi  Mkoa wa Ruvuma  naye akatoa maelekezo kwa Afisa Mteule wa Wilaya ya Nyasa  kutatua mgogoro huo wa kifamilia ambao mtoto alikuwa akimtaka mama yake kuondoka mara moja katika ardhi ya marehemu baba yake, kwa kuwa aliyemleta hapo amekwisha fariki dunia yeye anasubiri nini kuondoka katika maeneo ya baba yake.

Aidha alivitaja vitendo anavyofanyiwa na mwanae ni kuzuiliwa kulima mashamba aliyoachiwa na marehemu mume wake,kushambuliwa kwa lugha za matusi zilizomsababishia kuugua na kufukuzwa katika nyumba anayoishi, licha ya kuwepo wosia wa kimaandishi aliouacha marehemu mumewe wa kuwagawia kila mtoto eneo lake.

Mara baada ya kumuuliza mwanae Ferudhi Miteo amekiri kutenda vitendo hivyo kwa kuwa naye ana haki ya kumiliki ardhi ya Marehemu baba yake, na anaifahamu thamani ya ardhi, hivyo anafanya kila linalowezekana kumwondoa mama yao, ili aweze kumiliki ardhi hiyo ya baba yake, licha ya kuwa, wosia huu upo katika Ofisi ya Kijiji cha Mango na akakiri yeye binafsi anao.

Kwa upande wao Viongozi wa Vijiji ambao ni Telesphor Ndunguru wa kijiji cha Mango na Abeli lukuwi wa kijiji cha Songambele, wamekiri uwepo wa mgogoro huo na hawakujua sheria inasemaje kuhusu mali ya wanandoa, hivyo wamempongeza Afisa ardhi wa Wilaya ya Nyasa kuja kutatua mgogoro huo na kuahidi kuhakikisha kuwa kuanzia leo hakuna mjane atakayenyanyaswa katika Kijiji hicho na kumtaka Afisa huyo kutoa Elimu ya Sheria katika Mikutano ya Hadhara mara kwa mara ili kutatua migogoro ya ardhi pamoja na mirathi.

“Afisa ardhi Tunakushukuru sana kwa kutupa elimu hii kwa kweli tunakuomba siku nyingine uje, kwani unyanyasaji huu unafanyika kwa wajane wengi, hivyo elimu hii ikitolewa kwa watoto wetu itasaidia kupunguza manyanyaso kwa wajane, kwa kuwa tunafahamu haya yanatokea kwa kutokujua sheria”.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.