• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

NYASA KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA.

Posted on: January 10th, 2019

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa inatarajia kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambayo inatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni moja na nusu (1,500,000,000) itakayojengwa katika kitongoji cha Mtambo wa Lami kijiji cha Nangombo Kata ya Kilosa wilayani hapa ili kuwasogezea karibu huduma ya matibabu wananchi wa Wilaya ya Nyasa.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Dkt Oscar Mbyuzi wakati akiongea na wananchi wa Kitongoji cha Mtambo wa Lami, kijiji cha Nangombo Kata ya Kilosa, wakati akiwapa taarifa ya kukamilika kwa Taratibu kwa kuanza ujenzi wa majengo saba ya Hospitali ya Wilaya ya Wilaya ya Nyasa.

Dkt Mbyuzi alifafanua kuwa Wilaya ya Nyasa inakusudia kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya itakayojengwa katika kitongoji cha Mtambo wa lami katika kijiji cha Nangombo Kata ya kilosa ujenzi ambao unatarajia kuanza kesho kwa kusogeza miundombinu ya maji na kuanza ujenzi huo mara moja kwa kuwa tayari serikali imeshaleta fedha kiasi cha tsh (1,500,000,0000/=) bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujezi wa hospitali hiyo.

Aliyataja majengo yanayaoanza kujenga kuwa ni Jengo la utawala,Jengo la wagonjwa wan je(OPD),Jengo la stoo ya Dawa,Jengo la Maabara,jengo la vipimo vya mionzi(x-ray)Jengo la kufulia nguo(Laundry) na jengo la wazazi.

Aliongeza kuwa Taratibu zote za kuanza ujenzi zimekamilika ikiwa ni pamoja na kutangaza matangazo ya kutafuta fundi wa kujenga majengo ya hospitali hiyo na kuwashirikisha wananchi wa wilaya hii ili washiriki kikamilifu katika zoezi hili la ujenzi wa hospitali kwa kuwa kuna mafundi kujenga na wafanyakazi mbalimbali watahitajika na kipaumbele kitatolewa kwa wakazi wa wilaya ya Nyasa ili waweze kufanya kazi na kuongeza kipato kupitia kazi mbalimbali watakazokuwa wanazifanya katika eneo hilo la ujenzi.

Hapo awali Wilaya ya Nyasa ilikuwa haina Hospitali ya Wilaya hivyo ilikuwa inawalazimu wananchi kutembea umbali wa kilometa 66 kwenda  Hospitali ya Wilaya ya Mbinga kupata huduma za afya kwa kuwa hapa Nyasa kulikuwa na kituo cha afya cha Mbamba-bay ambacho kilikuwa hakiwezi kutoa huduma za afya zinazopatikana katika Hospitali za Wilaya.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia na Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwa amewajali sana wananchi wa Nyasa na hivyo kuwaondolea kero ya kupata matibabu mbali na nyasa hivyo aliahidi kusimamia vizuri ujenzi huu na kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuwaondolea kero wananchi wanaotembea umbali wa kilometa 66 kufuata huduma hizo kati hospitali ya wilaya ya Mbinga na kuongeza msongamano wa hali ya juu katika Hospitali hiyo.

“Namshukuru sana mheshimiwa Rais kwa kunipa fedha za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nyasa ambayo itawasaidia wananchi wangu kwa kuwa walikuwa wakiteseka wakisafiri takribani kilometa 66 kufuata matibabu katika wilaya ya mbinga kama unavojua mtu akiumwa atalazimika kutafuta nauli na kutembea umbali mrefu kufuata matibabu katika hospitali ya Wilaya hasa akina mama wajawazito ambao mara baada ya kukamilika hospitali ya Wilaya ya Nyasa itawaondolea usumbufu huo”.

Mhandisi Manyanya bado aliomwomba Rais kuona uwezekano wa kumwongezea  fedha za ujenzi wa kituo kimoja cha afya katika kata ya Kingerikiti tarafa ya Mpepo ambapo kuna ongezeko kubwa la watu na wanauhitaji mkubwa wa kituo hicho cha afya. wakati akiwa katika ziara ya siku kumi katika Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa hivi karibuni wananchi wa kata ya Kingerikiti kupitia kwa  Diwani wao wa kata ya kingerikiti mh. Alto Komba  walimwomba Mbunge Manyanya kuwajengea kituo cha afya kwa kuwa nao wanapata mbali huduma za afya.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.