• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

RC.IBUGE, WATAALAM WA AFYA TOENI ELIMU ENDELEVU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI

Posted on: July 14th, 2021

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameziagiza Halmashauri zote nane kupitia wataalam wa afya kusimamia kutoa elimu ya kujikinga na  maambukizi ya wimbi la tatu la corona.

RC Ibuge ametoa maagizo hayo wakati anazungumza na  wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma ngazi ya Mkoa na wilaya zote kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Amesisitiza elimu endelevu ya kujikinga kabla ya kuugua  corona itolewe kwa wananchi ikiwemo kuvaa barakoa,matumizi ya kunawa kwa sabuni na maji titirika na kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.

“Nimepita na kuzunguka baadhi ya maeneo mjini Songea,nimeona wananchi wameacha zile hatua ambazo tulikuwa tumezichukua katika wimbi la kwanza mfano,nje ya maeneo ya huduma,ndoo hazina maji wala sabuni,tukasimamie kuwaelimisha wananchi kwa sababu kujikinga ni gharama ndogo kuliko kutibu’’,alisisitiza RC Ibuge.

Amesisitiza kuwa corona ipo nchini,ingawa amebainisha kuwa katika Mkoa wa Ruvuma tishio la corona sio kubwa,hata hivyo amesema hakuna mipaka iliyofungwa  hivyo kuna mwingiliano mkubwa wa watu kusafiri na kuingia ndani ya Mkoa wa Ruvuma hivyo elimu endelevu ya kujikinga na corona isimamiwe ipasavyo kwa wananchi.

“Suala la  kujikinga ni rahisi kuonekana halina umuhimu kama madhara bado hatujayaona,sote tumekuwa tukisikia maelekezo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya na kupitia viongozi wa kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wimbi la tatu la corona tayari lipo nchini tuchukue tahadhari’’,alisema RC Ibuge.

Takwimu kutoka Wizara ya Afya zinaonesha kuwa hadi sasa Tanzania ina wagonjwa wa corona 408 waliothibitika kutoka baadhi ya mikoa hapa nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Julai 14,2021 

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.